Health&Food

Hivi ndivyo kichanga hukua katika tumbo la mama mjamzito toka wiki ya kwanza hadi kuzaliwa

on

Kwanzia wiki ya 1 hadi ya 4

 • kichanga hukua kwa kasi sana
 • kondo la nyuma hutengeneza chupa ambayo hujaa maji ambayo mtoto hukaa huko( nyumba ya mtoto) kitaalamu huitwa amniotic sac.
 • moyo huanza kutengenezwa na mapigo ya moyo huwepo
 • Miguu huanza kutengenewa.
 • mfumo wa fahamu huanza kuundika

Kwanzia wiki ya 4 hadi ya 8

 • Seli hali za mwanadamu huzalishwa kwa wingi sana
 • kichwa na baadhi ya maeneo ya uso huanza kutengenezwa.
 • baadhi ya viungo muhimu vya mwili kama figo,ini na mapafu huanza kutengenezwa
 • sehemu za siri za nje huanza kuundika ila huwezi kujua kama ni uke au uume.
 • huanza kusogea sogea au kusogeza miguu,mwili au kichwa chake ( kucheza)
 • huonekana katika kipimo ya Utra sound kwanzia mwenzi wa 6.

Kwanzia wiki ya 8 hadi ya 12

 • Jicho huanza kuundika
 • figo huanza kufanya kazi pia kwanzia wiki ya 10 mtoto huanza kukojoa.
 • Damu yake huzunguka kikamilifu kwenye mwili wake
 • Sehemu zake za siri hujulikana yaani kama ni wakiume utaona uume wake au kama ni wakike utaona uke wake.
 • hucheza kwa uhuru

Kwanzia wiki ya 12 hadi ya 16

 • mifupa huanza kuundika
 • sehemu ya juu ya mdomo huunganika na sehemu ya pua
 • nywele huanza kutokeza
 • huanza kutoa haja kubwa(meconium)

Kwanzia wiki wa 16 hadi wa 20

 • Mama huanza kusikia mtoto anacheza
 • mafuta meupe huanza kukaa kwenye ngozi yake
 • kucha huanza kuundika
 • ngozi huanza kubabuka na kujitengeneza upya.

Kwanzia wiki wa 20 hadi wa 24

 • mtoto husikia sauti
 • karibia ya viungo vyake vya mwili vyote hufanya kazi
 • ngozi yake huwa nyekundu na hujikunja
 • mtoto huwa na kipindi cha kulala na kipindi cha kucheza

Kwanzia wiki ya 24 hadi ya 28

 • macho hujifungua
 • anauweza¬† kuzaliwa na kuishi
 • uhemaji wake huwa umeimarika

Kwanzia wiki ya 28 hadi ya 32

 • nywele nyeupe huisha kwenye uso wake
 • mapumbu hutoka kwenye eneo la kiunoni na hushuka kwenye eneo lake.
 • mtoto huweza kuhifadhi mafuta na madini ya chuma

Kwanzia wiki ya 32 hadi ya 36

 • mafuta huongezeka kwenye mwili wa mtoto
 • nywele huisha kwenye mwili wa mtoto
 • nywele za kichani hurefuka
 • masikio huwa laini

Kwanzia wiki ya 36 hadi 42

 • mtoto anazaliwa
 • fuvu la kichwa limekuwa imara.

 

Mtokambali 728x90

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *