Cellebs

Mfahamu Wyne Rooney

on

 

              
Kuzaliwa:October 24,1985
Mahali:Croxteth
Uzito:82.7kg
Urefu:1.76M
Watoto:Kai Wayne Rooney
Klay Anthony Rooney
Kit Joseph Rooney

WASIFU WA WAYNE ROONEY
Wayne Rooney alizaliwa huko Croxteth, Liverpool.Alilelewa na wazazi wake Jeanette na Wayne pamoja na wadogo zake wawili wa kiume Graham na John.Kama ilivyokuwa kwa wavulana wengine katika mji wao ilikuwa ni ndoto ya Wayne kuwa mchezaji wa mpira wa miguu. Akiwa na miaka 9 alijiunga na academy ya klabu ya Everton.

Akiwa na umri wa miaka 16 tu,Wayne alijitangaza mwenyewe kwaenye dunia baada ya kufunga goli dakika ya mwisho ya mchezo, goli ambalo lilihitajika kuimaliza Arsenal ambayo haikufungwa michezo 30.Goli ambalo lilimfanya kuwa mfungaji bora mdogo zaidi katika ligi ya mabingwa Ulaya.Wayne alisaini mkataba na Manchester United August 2004,ulikuwa ni uhamisho ulio vunja rekodi ya dunia kwa kuwa na ada kubwa kwa kijana mdogo kama Wayne.

Wayne aliendelea kuwa nyota wa ulimwaengu kwa kushinda idadi kubwa ya mataji akiwa na klabu ya Manchester United.

KALENDA YA MATUKIO YA WAYNEY ROONEY
January 2016:Wayne alivunja rekodi ya ligi ya mabingwa Uingereza ya kuwa na magoli mengi akiwa na timu moja.
ushindi wa Wayne dhidi ya Liverpool kwenye uwanja wa Anfield ulimfanya afikishe goli la 176 akiwa na na Manchester United na kuvunja rekodi ya Thierry Henry.

September 2015:Wayney alikuwa mfungaji wa muda wote Uingereza.
Wayne alikuwa mfungaji wa muda wote Uingereza baada ya kufunga goli la 50 la kimataifa kwenye ushindi wa 2-0 dhidi ya Switzerland kwenye uwanja wa Wembley.

January 2015:Mchezaji bora wa  Uingereza kwa mwaka 2014.
Wayne alitangazwa kama mchezaji bora wa mwaka 2014 Uingereza.
Hii ni baada ya kupigiwa kura na mashabiki zake na ilikuwa mara yake ya tatu kushinda tuzo  hiyo

August 2014:Wayne alitangazwa kuwa nahodha wa Uingereza.
Roy Hodgson alimtangaza Wayne kama nahodha wa timu ya taifa ya Uingereza.

August 2014:Wayne alitangazwa kuwa nahodha wa Manchester United:
Baada ya mafanikio aliyoiletea klabu Wayne alitangazwa kuwa nahodha wa Manchester United.

February 2014: Wayne alisaini mkataba mpya.
Wayne alisaini mkataba mpya wa miaka mitano na Manchester United ndiye mchezaji ambaye anaongoza kwa kufunga magoli mengi katika klabu ya Man United.

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *