Cellebs

HISTORIA YA VANNESA MDEE a.k.a V. MONEY

on

Vannesa Hau Mdee ni TV presenter Radio presenter pia ni mwandishi wa nyimbo na mwimbaji amezaliwa tarehe 7 mwenzi wa 6 mwaka 1988 Ni msichana ambaye alianza kupenda mziki tangu akiwa mdogo, baba yake alikuwa mwandishi wa habari baadaye akawa balozi katika nchi ya Kenya na Ufaransa kisha baadaye alirudi jiji Arusha nyumbani kwake.

Vannesa amesoma katika chuo cha Catholic University of East Africa huko alisoma sheria ngazi ya degree, baada ya baba yake kufariki aliamua kuanza kufuata malengo yake na ndoto zake hapa duniani, alipata nafasi ya kushiriki katika MTV Vj ambapo aliweza kupata kazi hapo na kuanza rasmi kuwa mtangazaji katika kituo cha TV cha MTV.

Mwaka 2011 V Money alipewa nafasi ya kufungua shindano la Tusker CECAFA Cup, hapo ndipo kipaji chake cha kuimba kilianza kuoneka na Producer kutoka BHitz music group bwana Hammy B na kusaini rasmi kufanya kazi na V Money. Kisha safari yake ya muziki akaanzia hapo. Akiwa chini ya BHitz alishirikishwa katika nyimbo ya AY inayoiwa  Money kisha baadaye alishirikishwa tena na Ommy Dimpo katika nyimbo yake ya me and  you ambayo ilipata tuzo ya nyimbo bora ya mwaka.

Nyota yake iizidi kung’aa mwaka 2012 alitoa nyimbo  yake ya kwanza inayoitwa “closer” ambayo watu walidownload mara 30000 kwa wiki ya kwanza kitu ambacho hakijawahi kutokea katika muziki wa bongo fleva, 2013 Alitoa nyimbo yake ya pili comer over ambayo ilifanya vizuri sana katika muziki wa Afrika hadi Vannesa aliweza kuperfom katika Tuzo za Nigeria ilitengeneza na Producer Nahreel wa The Industry kisha 2014 alitoa Hawajui pia 2015 alitoa Never ever na ambazo  zilimuweka katika chati mbalimbali Africa na Duniani.

Vannesa mdee ameshiriki tuzo 18 hadi sasa na ameshinda tuzo 9

Mtokambali 728x90

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *