Cellebs

Mfahamu kiundani Msanii kutoka Nigeria mwanadada Tiwa Savage

on

Tiwatope  Savage Balogun amezaliwa tarehe 5 mwenzi wa 4 mwaka 1980 katika eneo la Ikeja huko Lagos Nigeria ni mwandishi wa nyimbo, mwimbaji na muigizaji. Baada ya kufikisha miaka 11 walihamia Wingereza kisha baadaye walihamia Marekani amehitimu shahada ya Uongozi wa biashara katika chuo kikuu cha Kent. Alianza kufanya kazi katika Royal Benk huko Scotland amefanya back vocal za wasanii maarufu duniani akiwemo Mary J Blige. Aliamua kurudi chuo cha Berklee collage of music na kusoma maswala ya muziki akiwa na miaka 27.

 

Mwaka 2016 Savage alishiriki katika The Tax Factor huko Wingereza ameshiriki mashindano mengi sana ya muziki mwaka 2009 Kampuni ya Sony music ilimsaini na kufanya kazi na wasanii kama Kat de Luna, Akon, snoop Dog kwa kuwaandikia nyimbo zao. Mwaka 2011 alifanikiwa kuhost show ya Nigerian Idol na kushiriki katika movie ya For colors girl na yeye ni balozi katika kampuni ya pepsi, forte oil na maggi

Mwaka 2012 alianzisha record label yake mwenyewe inayoitwa 323 Entertainment na pia alijiunga na Don Jazy na kuanzisha Mavin Record mwaka 2013 alitoa albamu yake ya kwanza inayoitwa Once upon a time ambayo ilikuwa na mchanganyiko wa nyimbo zinahusu maisha yake ya mambo ya siasa katika bara la Africa. mwaka 2014 ulikuwa mzuri sana kwake kwani alifanikiwa kutoa nyimbo kama love in yellow, wanted na turn in up pia alishirikishwa katika nyimbo kama Dorobucci, DSTV Africa rising Compain nyimbo hiyo alifanya pamoja na Davido, Mi Casa, Sarkodie. Pia mwaka 2016 ameweza kusainiwa na Record label kubwa duniani inayoitwa Roc Nation chini mmliki Jay Z .
Ameshinda tuzo 15 katika ya tuzo zaidi ya 30 alizoshiriki.

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *