Cellebs

Ifahamu historia ya Mchekeshaji maarufu Tanzania Mc Pilipili

on

Amewahi kuwa mwalimu lakini amefanya hiyo kazi hiyo kwa sababu mama yake ndiye alipenda afanye hiyo kazi iliacha kazi hiyo kwa sababu yeye alipenda kuchekesha sana watu, alifundisha miaka 6 huko Tanga, Dodoma anasema kazi ya ualimu aliifanya tu ili mkono uende kinywani mwaka 2006 baba yake alifariki na yeye kuamua kufanya kazi ya uchekeshaji kwa sababu ya majukumu pia alipenda sana kuchekesha anaseme kwamba usifanye kazi kwa kuangalia pesa fanya kazi kwa kuangalia moyo wako.

Akiwa mwalimu alichukua sehemu ya mshahara wake na kusafiri hadi hadi nairobi kuhudhuria show ya churchill raw aliomba nafasi ya kuperfomaliipata na alimiliki jukwaa kiasi kwamba Erick Omondi alimkubali sana.
Kitu ambacho anajivunia na kiligundulika hadi shuleni ni kwamba kipaji chake cha kuchekesha kiligundulika toka akiwa shuleni na alipomaliza form four alipewa chet cha special talent. Mwanzoni alipoanza kuchekesha alianza kubadilisha nyimbo za bongo fleva kuziimba kigogo  pia baada ya kuona mikoani hapati hela ya kutosha aliamua kuhamia Dar es salam.

Akiwa Dar alianza kufanya kama mtu wa kawaida alikodi chumba na kulala chini na alikopa laki tatu ili anunue godoro ila hakununua godoro tena hivyo aliamua kutengeneza business card na logo yake. Jina la pilipili alipewa na watu wa dodoma na watu wa msalato hii ni kwa sababu alikuwa mc katika masherehe pale inapofika muda wa kula anavaa kaptula na shati la shule watu ndio wakampatia hilo jina.

Kwa sasa anafanya matangazo ya biashara  kama lile la kampuni ua kupatana.com pia ni mtangazaji wa radio na TV anamiliki biashara zake za chakula. Akiwa anawashauri vijana alisema kwamba  ukitaka kufanya kitu cha mafanikio si lazima uombe ridhaa kwa watu.

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *