Cellebs

Mfahamu kiundani zaidi mtayarishai wa muziki na msanii Nahreel

on

Amezaliwa tarehe 12 mwenzi wa kumi na mbili mwaka 1989 katika mkoa wa Dar es salam  ni msanii, mtayarishaji wa muziki, na mjasiriamali. Jina lake kamili anaitwa EMMANUEL MKONO  jina lake maarufu ni NAHREEL ambaye amefanya nyimbo nyingi bora sana hapa Tanzania na Africa kwa ujumla.

Akiwa na miaka kumi na nne baba yake alimnunulia kinanda na mwalimu wake wa masomo za ziada akaanza kumfundisha namna ya kupiga kinanda na hapo ndipo kijana huyu alianza kuvutiwa na muziki na kuanza kufanya muziki. Alianza maswala ya muziki katika studio ya KAMA KAWA akiwa kama mtayarishaji wa muziki msaidizi ambapo alifanya kazi hapo kwa muda miaka miwili. baada ya hapo alinda India kwa ajili ya masomo.

Alitengeneza nyimba ya Riz One ambayo ilionekana nyimbo ambayo imeuza sana mwaka 2009 na kumfanya arejee Tanzania na kufanya kazi na Izzo Biznez. mwaka 2011 alimaliza elimu yake huko india  ambapo alikutana na rafiki Aika baadaye kuja kuwa mpenzi wake na kuanza harakati za kuanza muziki. Aika alisema kwamba walitokea kupendana baada ya kujua kwamba kijana ni mtayarishaji wa muziki na Aika yeye anapenda kuimba hivyo wakafanya kollabo.

Mwaka 2014 alifanikiwa kufunguwa kampuni yake mwenyewe pamoja na studio yake mwenyewe. Studio ilikuwa inaitwa Pr Managment na The Industry of School of Music(TISM)  Hii kampuni imeweza kufanya project nyingi na wasanii pia Nahreel ameweza kufanya kazi ya kundi la WEUSI ambapo lina wanamuziki kama Joh Makini,Nikki wa pili, Bonta na G nako amefanya kazi na Joh Makini toka mwaka 2007. Baada ya kuachana na kundi la PAH ONE kijana huyu aliamua kutengeneza kundi la NEVY KENZO ambalo limetoa nyimbo kama GAME ambayo imefika nafasi ya kwanza katika chat za MTV BASE. Mwaka 2014 alipata tuzo ya mtayarishaji wa muziki Bora katika tuzo za KTMA.

NYIMBO ALIZOFANYA;

 • Stimu zimelipiwa – Joh Makini (2010) (kili awards won best hiphop song of year)
 • Tanzania – Roma (2008)
 • Tanzania – kala jeremiah (2008)
 • Niaje ni vipi – joh ft nikki (2008)
 • Mziki huu – Izzo Bizness (2008)
 • Nakabaa koo – Izzo Bizness (2008)
 • Kiujamaa – nikki wa pili (2011)
 • RiziOne – Izzo Bizness (2011) (kili awards 3x nom)
 • Ghetto – Pah One (2012)
 • Amatita – Pah One (2011)
 • You – Pah One (2011)
 • I wanna get paid – Pah One (2012)
 • Kuwa na Subira – Rama dee (2012)
 • Zawadi – Vinega (Anti-Virus) (2012)
 • Kila kitu nyerere – Bonta (2011)
 • Usinibwage – Aika and Nahreel (2013)
 • Come Over – Vanessa Mdee (2013)
 • Chelewa – Navy Kenzo (2013)
 • Nje ya Box – Nikki wa pili ft Joh Makini and Gnakko (2013)
 • Gere – Weusi (2014)
 • Namchukua – Shilole (2014)
 • Naogopa – Gosby ft Ommy Dimples(2014)
 • Kolo kolo – Mirror (2014)
 • Sukido – Quick Racka ft Barnaba (2014)
 • Malele – Shilole (2014)
 • Hamjui – Vanessa Mdee (2014)
 • Aiyola – Navy Kenzo (2014)
 • Switch on Jingle – Airtel Tanzania (2014)
 • Safari – Nikki wa pili ft Johmakini, Vanessa Mdee, Jux, Aika & Nahreel (Navy Kenzo) (2014)
 • Moyoni – Navy Kenzo (2014)
 • I just wanna love you – Navy kenzo (2014)
 • Nobody but me – Vanessa Mdee ft KO (2015)
 • Nusu Nusu – Joh Makini (2015)
 • Nana – Diamond Platnumz ft Mr Flavour (2015)
 • Zigo – Ay (2015)
 • Mfalme – Mwana fa ft Gnakko (2015)
 • Game – Navy Kenzo ft Vanessa mdee (2015)
 • Looking for you – Jux (2015)
 • Laini – Gnakko ft Nikki wa Pili (2015)

Mwaka 2016 na 2017 Yeye pamoja na mpenzi wake Aika wameweza kuvuka mipaka ya nchi ya kufankiwa kusikika Africa na Duniani kwa ujumla wameweza kufanya tamasha katika nchi nyingi Africa na ulaya ikiwemo nchi ya Israeli pia wameweza kunyakua tuzo mbalimbali katika kipindi hiki. Wamefanikiwa kuanzisha record label yao inayoitwa The Industry na tayari wameweza kuwasimamia wasanii wawili ambao ni Wildad na Rasaree

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *