Cellebs

Historia ya mwanadada Hellen Downson

on

Hellen Downson ni mtanzania ambaye amezaliwa tarehe 18 mwenzi wa 11 mwaka 1986 mwenye umri wa miaka 29 katika Jiji la Dar es salam eneo la Kijitonyama. Elimu yake ya shule ya msingi ameipata katika shule ya msingi Muhimbili kisha St. Mary’s school akimalizia darasa la saba, O-level amesoma shule ya St. Mary’s na A-Level amesoma katika shule ya Shaban Robert akichukua combination ya HGL.

Baaada ya hapo alihamia Kenya kwenda kusomea maswala ya Ujasiriamali ngazi ya shahada katika chuo kikuu cha United State International University akiwa chuoni alikuwa akishughulisha na maswala ya mitindo na uigizaji, baadaye alirudi Tanzania na kushiriki katika mashindano ya Miss Universe na kushinda Taji hilo. Alipewa scholarship ya kwenda kusoma maswala ya Uigizaji nchini Marekani. Alifanya maswala ya mitindo na uigizaji lakini hakufanikiwa alirudi Tanzania tarehe mwenzi wa 8 mwaka 2012 hivyo wazazi wake walimlazimisha afanye Interviews katika makampuni mbalimbali ila hakufanikiwa.

Aliamua kuanza biashara ya kutengeneza Sabuni mteji wake ulikuwa ni laki mbili mbinu za kutengeneza sabuni alisoma kwa njia ya You tube, wazazi wake walimshauri akosome kabisa jinsi ya kutengeneza sabuni kwa sababu Bidhaa zake zilikuwa chini ya kiwango. Aliamua kutafuta darasa online na kumpata mwalimu kutoka Malaysia mwaka 2013 kwa ada ya dola 6000 kwa muda wa mienzi mitatu na kujifunza maswala ya shampoo, lotion za mbu na sabuni za mbu.

Baada ya kurudi Tanzania baba yake alimpa sehemu ya kutengenezea sabuni na mafuta hapo hapo nyumbani, SIDO , TBS na TFDA  walikuja wakakagua kisha wakamwambia aendelee kutengeneza bidhaa zake na zingine alikuwa akiagiza kutoka Malaysia ambao  ulikuwa ukimgharimu milioni 7.

kampuni yake ya Nuya Hellen na yeye Aliamua kuhamia Zanzibar baada ya kuona ugumu  wa kupitisha bidhaa katika bandari ya Dar es salam na Kuona urahisi wa kupitisha bidhaa katika bandari ya Zanzibar, Alianza kutengeneza sabuni zake na mafuta yake nyumbani kwa muda wa mwaka mmja na kwa sas anamiliki duka moja Zanzibar na stoo 5 huku akitarajia kufungua Duka lingine Dar es salam. Mwaka huu Jarida la Forbes limemuweka katika orodha ya vijana 30 Africa wanaotarajiwa kuwa matajiri Africa.

Mtokambali 728x90

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *