Uncategorized

HISTORIA YA MWANA FA NA HARAKATI ZAKE KIMUZIKI

on

Amesoma katika shule ya msingi Mdote huku Tanga baada ya kumaliza elimu ya msingi alijiunga na Shule ya sekondari Tanga. Mama yake alifariki akiwa na miaka 16 pia baba yake alimuacha akiwa mdogo sana hivyo hajawahi ishi naye.

Ni miaka 13 tangu FA kuwa katika chati ya Bongo fleva mbali na muziki  anapenda sana kucheza mpira wa miguu na mpira wa pete. Katika ukuaji wake amekaa na bibi zake na mashangazi zake. Alikaa kwa Ant yake mmja ambaye watoto wake walikuwa wakirap mtaani walikuwa na kundi lao linaitwa QGS Quit Ganster Chronic yeye aikuwa akikariri mashairi yao.

Alivyoenda shule Tanga alikutana na jamaa zake wakatengeneza kundi linaloitwa Black Skins ambalo alikuwa pamoja na Rob Gaz, Adam Geva walikuwa wakishindanishwa mara kwa mara na Raff Nigers chini ya marehemu Steve 2 K. Baada ya kumaliza shule Tanga alirudi na kuanza kuandika tuu mistari.

Bahati nzuri walikuwa wakiishi mtaa mmja na Dj Bonnie Love alimsumbua sana Bonnie Love kuhusu kurekodi ila baadaye DJ BONNIE alienda kusoma degree ya Sound Engineering kwa muda wa mienzi kumi na nane alivyorudi walianza kurekodi.

Akiwa anamsikiliza Mully B katika kipindi  Bongo fleva alishangaa kusikia nyimbo yake ya ingekuwa Vipi imepigwa na watu wakaomba irudiwe. Kwa siku 5 ilipigwa mara 75 katika vituo mbalimbali vya redio hapa nchini.

Mwana FA anasema kwamba yeye anafanya muziki kwa sababu anapenda na hii ndio sababu inamfanya asishuke kwenye chati. Nyimbo zake ambazo anazipenda ni kama vile Ingikuwa vipi mimi na mabinti damudamu pia bado niponipo pia wasanii wa zamani ambao  anatamani warudi kwenye muziki ni Ngwear, Solo thang na kwanza unity.

Nyimbo zake ambazo zimepigwa sana katika radio na Tv hapo bongo anasema ni pamoja na Asanteni kwa kuja,Yalaiti,bado nipi nipo na habari ndio hiyo.
Baada ya kutofautiana na Hammy B toka 2013 Josh ambaye ni rafiki wao wa karibu aliwaambia watatue tofauti zako mwaka 2015 mwanzoni  na sasa wanapiga kazi pamoja. Maproducer aliofanya kazi nao kwa muda mrefu ni Bonnie Love,Hammy B na P Funk.

Mtokambali 728x90

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *