Cellebs

Ifahamu historia ya muigizaji Rammy Galis

on

 

Rammy Galis  anasema kwamba mama yake ni msomali baba yake ni mbrazili amezaliwa mwaka 1990 tarehe saba mwenzi wa kumi jijini Dar es salam. Amesoma elimu yake ya sekondari na msingi katika mkoa wa Dar  es salam, chuo amesoma mkoa wa Singida kinachoitwa TLA mwaka 2010 mpaka 2012  alichukua uhasibu katika ngazi ya cheti baada ya  kumaliza alirudi Dar es salam. Baba yake anawatoto kumi .Alianza kupenda kufanya sanaa ya kuigiza miaka mingi ila alishindwa kwa sababu ya masomo. Baada ya kumaliza chuo alikutana na Hemed Suleman ila kwa kipindi hicho hakuweza kufahamika kwa sababu Hemed bado naye alikuwa hajawa maarufu ndio alikuwa anaanza kuigiza.

Alikutana na kanumba katika Bar moja kisha akiwa anaenda toilet walipishana naye kisha wakapiga story mbili tatu Kanumba akamualika wakae katika meza moja na Kanumba alimwambia kwamba anafanana sana na yeye kisha aliamua kumchukulia Rammy kama mdogo wake. Baada ya Kanumba kufariki alisafiri mpaka Nigeria kisha alikutana na producer mayosa anasema kwamba ofisi za Kanumba zilifungwa karibuni mwaka mmja kutokana na migogoro ya kifamilia hivyo steps walimchukua na yeye alianza kufanya kazi chini ya steps. Katika mkataba wake steps wanategemea Movie tatu kila mwaka kutoka kwake.

Alipata kazi katika Bandari ya Dar kwa muda wa mwaka mmja na nusu kisha akaacha hii ni baada ya kufanya movie na Kanumba kisha steps walimpa mkataba wa kufanya kazi hivyo akaona kipata cha uigizaji ni kikubwa kuiliko cha kazi. Mwaka 2012 mwishoni alitoa movie yake ya kwanza inayoitwa LOVE AND POWER pamoja na Kanumba.Rammy anasema aliwahi kwenda Ghana kwa ajili ya Holiday alienda kwenye shirikisho la filamu Ghana ili kujaribu kupata nafasi ya kufanya movie huko alionyesha kazi zake na kukutanishwa na producer mmja ambaye alikuja Tanzania na kufanya kazi naye.

Mtokambali 728x90

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *