Cellebs

Historia ya Muigizaji Nisha

on

Amezaliwa miaka 27 iliyopita ni mtoto wa pili kwa mama kati ya watoto watatu pia ni mtoto wa pili kati ya watoto tano wa baba. Baba yake ni mwanajeshi na mama ni mfanyabiashara, amesoma katika shule ya msingi Jamuhury kisha Sekondari alisoma katika shule za St Vicent na Alharimaini. Nisha anamtoto mmja wa kike aliyejifungua akiwa na umri wa miaka 17.

Anaitwa Salma Jadu alivyokuwa mdogo alikuwa akipenda filamu za kihindi na kumpenda muigizaji anayeitwa Nisha ndiyo maana yeye mwenyewe amejiita Nisha. Baada ya kumaliza kidato cha nne alifaulu ila familia ilikuwa inashida kubwa ya hela hivyo alishindwa kuendelea na masomo ili kumruhusu mama amsomeshe mdogo wake wa kiume, Aliingia mtaani na kuanza kufanya biashara mbalimbali. Aliwahi kwenda Chini ili kufanya uchunguzi wa biashara bahati nzuri akaweza kuanza biashara bila hata kumaliza uchunguzi.

(Kwa  historia za wasanii mbali mbali na makundi makubwa ya m uziki Ulimwenguni tembelea>>>>>> mtokambali.com)

Peace of mind ndiyo filamu iliyo mvutia yeye kuigiza alikutana na Mobb Mpangala na kumuingiza katika filamu iliyoigizwa tena. Kisha safari ikaanza kwa kufanya marudio ya filamu hiyo. Alianza kufanya kazi na Game first quality kisha RJ Company kwa muda wa mwaka mmja baada ya hapo aifungua kampuni yake ya Nisha Production yenye miaka minne hadi sasa. Alisitisha kidogo swala la kuigiza na kwenda China kusomea maswala ya Ujasiriamali.

Filamu yake ya Kiboko Kabisa ndiyo filamu aliyomuingizia hela sana kwa kuuza zaidi  ya asilimia 64% . Ni balozi katika katika kituo cha watoto wanaoishi katika mazingira magumu kinachitwa Tumaini kilichopo jijini Dar es salam. Kampuni yake asilimia 80 ya kila filamu anayoifanya waigizaji huwa ni chipukizi hii ni ili kuinua vipaji vya Waigizaji wachanga.

(Kwa  historia za wasanii mbali mbali na makundi makubwa ya m uziki Ulimwenguni tembelea>>>>>> mtokambali.com)

Mtokambali 728x90

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *