Cellebs

HISTORIA YA MTANGAZAJI WA CLOUDS FM ADAM MCHOMVU aka BABA JOHNNN

on

 

Adam mchomvu anamtoto mmja wa kiume anaitwa Brairon yeye ni single parent. Ni mtangazaji pia ni msanii miondoko ya HipHop ananyimbo kama bwana shamba john john ambazo zimefanya vizuri sana. ni mtangazaji wa Clouds Fm katika kipinda cha xxl na Soso fresh.

alianza kufanya muziki hata kabla hajawa mtangazaji, akiwa anasoma Uganda Ntinda view akiwa huko alikuwa akihost matamasha mbalimbali shuleni na alianza kazi za presentation Uganda  katika redio inayoitwa Uganda Capital Fm.Kipaji chake cha kiligungulika pale akiwa klabu huko Uganda kulipotokea ugonvi hapo ndipo Izack Mumenya akamwambia anasauti nzuri na kumpa dili ya kubadilisha tangazo kwa lugha ya kiswahili hilo ndilo lilikuwa tangazo la kwanza kufanya.

Baada ya kumaliza masomo Uganda aliporudi Tanzania aliwaambia wazazi wake kwamba anataka kuwa mtangazaji mama yake alikuwa mgumu kuelewa lakini hatimaye alikuja kukubaliana naye. Alienda Dar es salam kusoma chuo cha utangazaji DSJ. Akiwa hapo chuo Clouds fm wakawa wanatafuta mtangazaji wa Africa Bambataa ndio akaingia katika kinyang’anyiro hicho. Jumla ya watu walioshiriki katika kinyang’anyiro hicho ni 4000 na yeye alishika nafasi ya pili katika shindano hilo.

Style yake ya utangazaji anasema huwa anatangaza kama anapiga story, pia anapoona watangazaji wengi wa sasa wanamuiga jinsi anavyotangaza anasema siyo mbaya ila ni vizuri mtu awe kama yeye yaani awe na kitambulisho chake mwenyewe. Ubunifu wake hupata usomaji wa vitabu na kufuatilia  vitu sana.Akiongelea kuhusu vijana wengi kufanya mziki anasema siyo vizuri watafute vitu vingine vya kufanya pia amewahi kuwa na beef na wasanii wa bongo fleva pia ni wasanii wanapenda kutafuta beef ili ziwakuze. pia hutumia mitandao ya kijamii kwa ajili ya kutangaza matangazo.

Kuhusu kutimiza malengo malengo yake anasema bado anahitaji kufanya kazi kuyatimiza. Adam Mchomvu amewahi kuwa program manger katika uanzishaji wa Mbeya Fm pia akiwa  anawaongelea watoto wa mtaani anasema kwamba ni wapambanaji, akiwa shauri vijana kuhusu kutimiza ndoto anasema kwanza sikiliza moyo wako unapenda nini kisha tafuta watu wanaofanya unachokipenda wafuatilie wanavyokitenda.

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *