Cellebs

HISTORIA YA MSANII WA NIGERIA YEMI ALADE

on

Yemi Eberechi Alade amezaliwa tarehe 13 mwenzi  3 mwaka 1989 ni mtoto wa tano katika familia ya watoto saba, elimu yake amepata katika shule ya St. Saviour British primary, kisha akasoma sekondari ya Victory Grammar school huko lagos na baadaye alichukua shahada yake ya geografia katika chuo kikuu lagos.

Alade alianza maswala ya muziki mwaka 2005 pale alipokuwa katika kundi la muziki lililoitwa Noty spices kipindi akifanya mukizi kama kundi hakusikika sana mpaka pale ambapo alishanda katika shindano la Peak Talent show mwaka 2009.Mwaka 2012 alisainiwa katika lebo ya Effyzie music group na alitoa nyimbo yake ya kwanza inayoitwa Ghen Ghen Love ilifanya vizuri kiasi chake huko kwao nchini Nigeria.

2013 mwishoni ndiyo mwaka ambayo msanii huyu alianza kupata airtime sana katika nchi za Africa, ulaya na Marekani. Alitoa nyimbo inayoiwa Bamboo kisha akatoa tena Jonny mwishoni mwa mwaka huo na kuteka sana nyimbo ilifanywa chini ya SELEBOBO na kushika chati sana katika nchi kama Tanzania, Kenya, Africa kusini, Zimbabwe, Ghana na Wingereza. Alade aliweza kutumbuiza katika jukwaa moja na Mary J Blige pia katika tuzo huko Nigeria mwaka 2013.

2014 Alade alishirikiana na wasanii mbalimbali kutoka Nigeria na kushiriki katika nyimbo ya “lights” hii ni kwa ajili ya kuhimiza watotot waende shule na wabaki shule kwa masomo pia alitoa video ya jonny ambayo iliangaliwa mara milioni 32.

Alade aliendelea kushika chati mwaka 2015 mwishoni na kibao chake kinachokwenda kwa jina la Na gode ambacho kimembwa kwa lugha ya kiswahili na kingereza  pia ametoa albamu moja hadi sasa.

ameshinda tuzo moja kati ya tuzo saba  alizoshiriki.

Mtokambali 728x90

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *