Cellebs

Mfahamu na fahamu harakati za msanii Maua Sama

on

Anaitwa Maua Salehe Sama jina hili ameridhi kutoka kwa bibi yake, amezaliwa Tanga tarehe 28/8/1994 baba yake alipata kazi katika chuo kikuu cha Ushirika Moshi ndipo yeye akahamia Moshi. Amesoma katika shule ya msingi Moshi pamoja na Kilimanjaro primary school elimu ya sekondari amepata katika shule ya Rau pamoja na Kiborolioni na hakufaulu form four. alipata Four ya 26.baada ya hapo alijiunga na chuo cha Ushirika na kusomea Certificate of microfinance baada ya hapo alichukua Diploma ya herprices kisha akasoma degree elimu yake ilimchukua miaka sita.

Muziki alianza akiwa sekondari na hicho ndicho kilichomfanya akashindwa kufaulu vizuri form four, alikuwa akirekodi pia kuwaimbia marafiki zake nyimbo za wasanii wengine pamoja na zakwake ila hakuwa kutoa nyimbo rasmi ambayo angepigwa redioni, baba yake alikuwa hapendi mwanae kufanya muziki hivyo alikuwa akifanya muziki kwa siri bila baba kujua.

Walijuana na Mwana FA baada ya kutoa nyimbo ya So crazy kisha dada yake na rafiki yake alichukua ile nyimbo na kwenda kumsikilizisha FA mwanafalsafa alimkubali sana kisha akaomba atumie nyimbo zingine za Maua Sama ili kuangalia kama kweli anajua baada ya hapo Gafla akiwa nyumbani alipigiwa simu na mwana FA kwamba aende Dar es salam kufanya nyimbo hakuaga nyumbani kama anaenda Dar.

So crazy ndio nyimbo ambayo ilianzisha safari yake ya muziki wake pia nyimbo yake ya let them know ambayo imempa tuzo ya KTMA kama nyimbo bora ya regge kisha Mahaba niue ambayo imemfanya ajulikane vizuri na kushika chati kubwa katika radio hapa nchini. Pia anatarijia kutoa albamu yake mwaka huu. Kwa sasa yupo chini ya THT na hii ni baada ya mkataba wake na FA kuisha na yeye kumshauri aende THT ili  kujifua zaidi.

Maua mwaka 2017 amefanikiwa kutoa ngoma yake inayowenda wa jina la main chek ambayo inatamba sana katika  chati mbalimbali hapa nchini

 

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *