Cellebs

Historia ya msanii Belle 9

on


Amezaliwa katika mkoa wa Iringa tarehe 9 mwenzi wa 9 baada ya muda kidogo baba yake alihamia Morogoro kikazi kipindi hicho Belle alikuwa mdogo sana,  Ni mtoto wa pili katika familia ya watoto watatu ambayo baba na mama wote ni wafanyakazi,  Amesoma Morogoro katika shule ya msingi Chamwino kisha akaenda Iringa kusoma elimu ya sekondari lakini hata hivyo hakumaliza shule ya sekondari hivyo aliishia kidato cha tatu sababu ya kuacha shule ni wazazi hawakuwa na uwezo wa kumsomesha pia muziki ulikuwa pia ni chanzo kingine katika kushindwa kufanikiwa kimasomo.
Akiwa shuleni alikuwa akipenda kuimba katika madisco, na mashindano ya talent kisha kupewa zawadi za pasi, feni.

Baada ya kuacha shule wazazi walimuuliza kwamba anataka kufanya nini, kisha akajibu muziki , wazazi hawakupenda yeye afanye muziki kwa sababu hawakuona faida ya yeye kuimba hivyo mama yake alimua kumtafutia kazi katika kiwanda cha tumbaku kama kibarua wa kupanga magunia kazi hiyo aliifanya kwa muda wa mwaka mmja, Pia amewahi kuuza mayai katika stendi ya Morogoro kwa mtaji ambao alipewa na mama yake ili aweze aweze kujikimu  katika mavazi baada ya hapo aliacha kisha mama akamtafutia kazi ya kuwa kondakta wa daladala kwa muda wa mwenzi mmja.

Katika harakati zake za kimuziki amewahi kuwa kundi moja na mwanamuziki Diamond Platnumz, safari yake ya kimuziki ilianza baada ya Dj Mull B kuja Morogoro akatengeneza kundi la muziki linaloitwa Moro tete wakawa wakirekodi nyimbo na kuzituma Dar es salam baada ya muda alijitoa kwenye kikundi hicho kisha akakutana na Mona Gensta, Alirekodi nyimbo tatu ambazo hazikusikika sana na aliporekodi nyimbo ya nne ambayo ni “Sumu ya penzi” ilimtambulisha rasmi katika muziki wa Bongo Fleva kipindi hicho chote alikuwa hajaacha kazi katika kiwanda cha Tumbaku.

Baada ya mafanikio aliyoyapata katika sumu ya penzi basi alimwambia mama yake kwamba anaacha kazi na mama alimkubalia, kwa mara ya kwanza alitumbuiza katika chuo cha Mzumbe na kupewa laki moja kisha rafiki yake alimkutanisha na Adam Juma na kutoa video ya Sumu ya Penzi kisha akaendelea kutoa nyimbo kali kama masogange na bagga muvi selfie ambazo zimefanya vizuri sana.

Belle 9 hatumii kilevi chochote pia kwa sasa amehamia kijito nyama Dar es salam hii ni kutokana na managment yake kukaa Dar muda mrefu pia shughuli nyingi za muziki hufanyia Dar.

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *