Cellebs

HISTORIA YA MSANII ALI KIBA

on

Ni msanii ambaye huwa anashindanishwa sana na Diamond Platnumz pia amejitahidi na kuweza kutoshuka katika muziki toka atoke ya kujulikana kama msanii mkubwa hapa nchini amewahamasisha vijana wengi sana kuingia

katika muziki na kuona nao wanaweza kutoka kwa njia ya muziki

Amezaliwa mwaka 1986 tarehe 26 mwenzi wa 11 ni mtoto wa kwanza kati ya watoto wa nne wa Saleh Omary Akifuatiwa na Abdukiba. Akiwa anasoma Shule ya Msingi Upanga alipenda sana kuimba katika talent show na masherehe mbalimbali hapo shuleni. Baada ya kumaliza Elimu ya A-level mwaka 2004 aliamua kuweka nguvu zake katika muziki rasmi na kutoa ngoma kama Maria.

Ali kiba akiwa na  Joket
2005 alipewa ofa ya kucheza mpira katika timu moja huko Uganda alikataa kwa sababu hilo lilikuwa siyo lengo lake la maisha hivyo aliendelea kukaza buti katika maswala ya muziki.
mwaka 2007 alitoa albamu ya Cindellela
Mwaka 2008 alitoa albamu ya Alikiba 4 real
2009 timu inayocheza ligi kuu ya Bongo African lyon walimtaka lakini hakuwa tayari.

Alikiba ameshirika katika nyimbo moja na R kelly katika project yake ya One8 ambayo ilichukuwa tuzo ya BET kama most inspirational song pia kiba mwaka 2014 alifanikiwa kuchukuwa tuzo tano za kili muziki awards na ngoma yake ya Mwana. Mwaka 2017 King Kiba ameweza kunyakua tuzo mbili za AFRIMA kupitia kibao chake cha Aje akiwa na M.I kama nyimbo bora ya mwaka ya Africs na pia  nyimbo bora ya kushirikiana ya Afrika.

 

Mtokambali 728x90

Recommended for you

3 Comments

  1. DUNSON DITANIUMZ

    November 8, 2016 at 7:28 am

    Ingiza maoni yako…Poa Poa

  2. Selemani angali

    November 15, 2017 at 8:24 pm

    Poa sana

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *