Cellebs

HISTORIA YA MSANII AKOTHEE

on


Ester Akoth, Ni mzaliwa wa Migori count ya Nyanza alihamia Mombasa baada ya ndoa yake kuvunjika, mdada huyu aliolewa akiwa na miaka 14 na kuzaa watoto watatu na mume wake wa ndoa. mtoto wake wa kwanza alimpata akiwa na miaka 14 mtoto wake wa pili alimpata akiwa na miaka 16 ambaye alikufa, mtoto wake wa tatu alimpata 18 na mtoto wake wa nne alimpata akiwa na miaka 20.

Akimwa na miaka 23,Baada ya kuhamia Mombasa alianza kufanya kazi ya ‘kuendesha matatu’ huku Tanzania tanzania huitwa daladala alifanya hiyo kazi kwa siku tatu baadaye aliacha na kuanza kuendesha Tax so alihamia katika kazi ya” tax driver” akiwa Mombasa alipenda sana kuucheza dancing katika klabu moja huko Mombasa japo kuwa aliishi maisha ya shida. Mzungu mmja katika klabu hiyo alimpenda jinsi anavyokatika kisha akamwalika holland kucheza katika Birthday yake.

Akiwa na miaka 24 alikwenda Holland katika party ya huyo mzungu, Akothee alilipwa kiasi cha dola 300 ambayo ni sawa na milioni 6 za Kitanzania baada ya kupata hizo ela aliamua kupanga nyumba na kuchukua wototo wake kutoka kwa babu yao ambako anasema waliishi kwa shida sana. Pia Akothee aliamua kununua tax yake mwenyewe ya kufanyia biashara alikuwa pia anatengeneza sabuni za maji ili kupata kipato pia kwa njia nyingine.

Akiwa amepanga aliamua kufungua Hoteli yake na alikutana muzungu mwingine ambaye alikuwa akipenda kula katika hoteli yake alingia katika mapenzi na yule mzungu kisha alimweka ujauzito na kwenda naye Swazland kisha allishi naye na ikafika mahali Mzungu akamwambia kwamba hawezi kumuoa hajajiandaa kuwa na maisha ya ndoa, ilibidi Akothee arudi Kenya hata bado hajajifungua.
Yule mzungu alimpa kiasi cha dola 10000 kwa ajili ya matumizi.

Alijifungua mtoto wake kenya mwaka 2008 na ile hela aliyopewa alinunua Noah na nyingine alilipa kodi ya nyumba. akiwa katika unyumba alipata kazi ya kwenda kumchukua mgeni mmja hotelini, alipombebea  mgeni huyo alitokea kumpenda kisha alimpa namba ya simu. Mgeni huyo alimjengea nyumba na kuishi kwa muda kisha wakaachana.

Muziki alianza kuimba mwaka 2013 rasmi studio chini ya producer wake TOTI alitengeneza ngoma yake ya kwanza inayoitwa nimechoka mpaka sasa ananyimbo saba, nyimbo zake zote saba anasema zimemuweka juu. Mwisho anasema kwamba Mungu kakupa akili ili uweze kufikiria na kupambana na maisha yake. Hakuna uganga wala illuminati.

Mtokambali 728x90

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *