Cellebs

HISTORIA YA MKONGWE WA MUZIKI AFRIKA PAPA WEMBA

on

 

Shungu Wembadio Amezaliwa mwaka 1949 tarehe 14 mwenzi wa 6 huko Lupefu katika nchi ya Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo alianza maswala ya muziki baada ya kujiunga na kundi lanaloitwa Zaiko Langa Langa mwaka 1974 akiwa pamoja na wasanii kama Bozii Boziana, Mohamed Ali na Georgeforeman na kufanya muziki wa staili yao ukiitwa Isifi lokole. mwenzi wa saba mwaka 1975 ndiyo jina lake lilianza kuwa maarufu kama Papa wemba

Mwaka 1975 mwenzi wa 11 Papa Wemba aliachana na kundi la Isifi lokole na kutengeneza kundi lake lililoitwa Yoka Lokole ambolo liliufikisha muziki wa Afrika katika sehemu kubwa duniani na walitoa nyimbo zao maarufu kama Matembele Bangui”, “Lisuma ya Zazu” (Papa Wemba), “Mavuela Sala Keba”, and “Bana Kin” (Mavuela Somo).

Katika eneo lake la nyumbani linaloitwa Matonge alitengeneza kundi la muziki kwa ajili ya kunyanyua vipaji vya muziki katika sehemu hiyo kwa vijana ambao wanapenda kuimba kundi hilo lilikuwa likiitwa Viva la Musica ilikuwa ni mwaka 1977 kundi hilo lilikuwa na wasanii kama  Kisangani Esperant, Jadot le Cambodgien, Pepe Bipoli and Petit Aziza. Koff Olomi kipindi hichi ndiyo alikuwa akitoka na kioo cha kilikuwa ni Papa wemba. katika kijiji kilichopo Matoge alipewa heshima ya uchifu hii ni kwa sababu ya kuwanyanyua vijana wengi katika mtaa huo.

Miaka ya 1980s alianza kufanya ziara za kimuziki Ufaransa akiwa pamoja na wasanii wenzake katika kundi la Viva la Musica na walitoa nyimbo zao kali kkam ‘Esclave” (1986), “Le Voyageur, Maria Valencia” (1992), “Foridoles, Dixieme Commandement” (1994), “Emotion” (1995), “Pole Position” (1996), “Bakala dia Kuba” (2001), and “Somo Trop” (2003).

Mwaka huu tarehe 24 mwenzi wa nne mwaka 2016 akiwa katika jukwaani FIMA akitumbuiza huko Ivory Coast alianguka ghafla na kuaga dunia hapo hapo. Amekufa akiwa na miaka 66.

Mtokambali 728x90

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *