Uncategorized

HISTORIA YA LEGENDARY WA GENGE JUA CALI

on

PAUL JULIUS NUNDA Amezaliwa tarehe tarehe 12 mwenzi wa tisa 1979 Eastland Nairobi wazazi wake wote wawili Doreen Onditi na Evansi Onditi walikuwa walimu. Alianza maswala ya kufanya muziki wa rap akiwa na miaka kumi pamoja na kaka yake anayeitwa Christopher Jua Kali alifahamika kuwa ni mpole na mtulivu.

Amesoma katika shule ya Ainsworth Primary School (Standards 1 to 6); Shepherds Junior Buruburu (Standards 6 to 8); Jamuhuri High School baada ya hapo alijiunga na   Kenya Christian Industrial Training Institute (K.C.I.T.I) Eastleigh ambapo alipata Diploma ya information and technology(I.T)

ALianza harakati za muziki baada ya kutemwa kucheza timu ya taifa ya mpira wa kikapu baada kuonekana kimo chake hakiruhusu. Mwaka 2000 Yeye pamoja na rafiki yake CLEMO  walianzisha studio yao ya kurekodi muziki inayoitwa CALIF RECORD hii ilimfanya kupata heshima kubwa kwa kaka yake Chris pamoja na wazazi kwa ujumla. Jua Kali alitamba sana kenya na africa mashariki kwa ujumla na kuutangaza mziki wa genge.

Nyimbo yake ya kwanza kutoa ni Ruka mwaka 2001 ikifuatiwa na nyimbo Nipe asali mwaka 2002. Mnamo mwaka 2004 alitoa nyimbo Kamata demu akishirikiana na PILIPILI kama kawaida ya wasanii wa Kenya ilimchukua muda ili kutoa albamu ambayo aliitwa JUACALI SEKTA aliitoa mwaka 2006.

Alitoa nyimbo inayoitwa  Kwaheri akishirikiana  Sainapei Tande-ilishinda cocacola pop star ilibamba sana  Kenya mwaka  2007. mwaka mpya 2008/2009 alitoa albamu inayoitwa Ngeli ya Genge. Alifanya matamasha  US na mataifa mengine.  mwenzi wa nane 2007, alikuwa kati wahamasishaji 100  katika nchi  Kenya na kuchaguliwa na The standard  newspaper.

Kaatika jukwaani Jua Cali, limetokana  na  California,sehemu ya huko Nairobi (kama jina Calif Records).
Ametoa nyimbo mpya aliyotengeneza na  producer wake mpya  Keggah anayekaa Marekani. nyimbo zake mpya, Karibu Nairobi na Kuna Sheng ambazo zote zimepokelewa vizuri na mashabiki wake.
Ni balozi wa Motorola, Orange mobile na pamoja mtaani.


Albums:
  • JuacaliSekta (October 2006:)
  • Ngeli ya Genge (December 2008)
  • TuGenge Yajayo(December 2013)
TUZO
ALIZOSHINDA
ALIZOSHINDANIA
Mtokambali 728x90

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *