Cellebs

Historia ya Kiss Daniel

on

 

Anidubge Oluwatobiloba Daniel maarufu kama Kiss Daniel ni mwandishi wa muziki, mwimbaji na mchekeshaji anaimba muziki aina ya Afro-pop amezaliwa mwaka 1992 huko Nigeria mtaa wa Ogun na kupata elimu yake ya msingi na sekondari huko huko baadaye alijunga na chuo kikuuu cha Federal na kutunikiwa shahada ya kilimo mwaka 2013. Wazazi wake walimsihi sana asome kwa bidii na anawashukuru wazazi wake kwa hamasa hiyo.

Alianza kuimba akiwa na miaka 11 kwa kutunga na kuimba nyimbo zinazohusu mambo ya chakula na baba yake alikuwa akimsaidia katika kumrekebisha uimbaji na utungaji, mwaka 2009 alikutana na msanii anayeitwa JABLESS alimsaidia Kiss Daniel kukuza kipaji chake na kuandika nyimbo ambazo zinauzika,

mwaka 2014 muziki wake ulikuwa sana pale ambapo alimwaga wino katika record labe ya G-WorldWide Entertainment na kutoa nyimbo yake ya kwanza inayoitwa “SHOYE” mwenzi wa 5 tarehe 1 mwaka 2014. Mwaka huo huo mwenzi wa tisa alitoa “WOJU” ambayo iliweza kufika top 5 ya chart nyingi Africa na iliweza kukaa wiki 11 katika chati kubwa ya M|TV Base Africa. 2015 Kiss alitoa nyimbo ya tatu inayoitwa “Laye” na mwaka huo huo alifanikiwa kunyakua tuzo mbili 2016 ametoa nyimbo ya “Mama” ambayo imefanya vizuri mara dufu zaidi katika chati mbalimbali ndani na nje ya Africa.

Source; wikipedia.org, http://www.takemetonaija.com

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *