Cellebs

HISTORIA YA KIMUZIKI YA MSANII RAPPER CHEMICAL

on


Alianza muziki akiwa kidato cha pili wakati huo alienda kwa producers wengi sana likini hakutoka kipindi hicho baada ya hapo alitoa ngoma ya struggle ilitoyotayarishwa na Duke chini ya M Lab aliifanyia video hiyo ngoma hapo kaka yake aliona mdogo wake anakitu na kuanza kumsupport.

Kaka yake aliona Chemical ameamua kufanya muziki kazi hivyo akaamua kumsimamia katika muziki wake, alitoa ngoma yake iliyomuweka kwenye chati nyingi hapa bongo inayoitwa sielewi iliyofanywa na producer maximizer ndipo jina lake likaanza kukuwa kama rapper wa kike hapa bongo.

Jina lake la chemical alipewa na Mesen Selekta baada ya kumuona dada huyu ni mkali sana katika kuchana, kwa sasa yupo chini ya Kazi Kwanza Entertainment anayomilikiwa na kaka yake,. Anasema kwamba alikuwa chini ya MJ Records lakini baada ya kumaliza form 4 aliacha kufanya muziki ndipo aiachana na Maco chali.

Changamoto alizokutana nazo ni wazazi kukataa afanye muziki pia watu kumdanganya watamsaidia pia malengo yake ni kuipeperusha bendera ya taifa, msanii anayemkubali na kumtamanisha yeye aingie katika muziki ni Young D hii ni kwasababu alimuona akifanya muziki toka akiwa mdogo na kufanikiwa. wasanii anaotamani kufanya nao kazi n Fid Q, young D na Roma.

Studio alizofanya nazo kazi mpaka sasa ni Defartality, MJ Records, Nahreel kwa sasa yupo chuo kikuu mlimani mwaka wa kwanza katika ngazi ya diploma ya sanaa na muziki. Anachokiamini mwanadada huyu ni kwamba muziki utamfanya avae, ale na aendeshe maisha yake.

Mtokambali 728x90

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *