Uncategorized

HISTORIA YA JUX NA HARAKATI ZAKE

on

Juma Jux aka JUX amezaliwa mwaka 1989 na kuishi na kukulia katika jiji la Dar es salam mpaka mwaka 2005 ambapo alianza harakati za muziki kama rapper. Mwaka 2008 alikutana na Cyril Kamikaze na Nigga flow wakatengene kundi la WAKACHA na kuwa na cheo cha makamu wa raisi wa kundi hilo.

Baada ya muda alianza kufanya kazi mwenyewe na kuredi katika studio ya AM Records kuredi nyimbo yake ya kwanza ambayo ni napata raha  na aliendelea kuwashirikisha wasanii kama kamikaze Mabeste. Stamina Vaneesa Mrap Mo rack na wengine.

Ni msanii wa miondoko ya R&B katika muziki wa Bongo fleva hapa Tanzania pia ni Mwanamitindo maarufu sana katika kanda ya Africa masharika. Mwaka 2014 alishinda tuzo ya KTMA kama mwanamuziki bora wa miondoko ya  R&B hapa Tanzania.

Vannesa Mdee ndiye mpenzi wake ambaye mara nyingi hupenda kuwa naye. Ametoa ngoma nyingi kama sisikii, ntasuri na mwaka huu ametoa nyimbo kali mbili ambazo zinafanya vizuri sana katika soko la kimataifa na kupigwa katika TV station kubwa duniani kama TRACE TV, MTV BASE nyimbo hizo ni looking for you ambayo ameshirikiana na Joh Makini na mpya ya sasa One more night ambayo inafanya vizuri pia.

Recommended for you

1 Comment

  1. Kelvin Julius

    August 30, 2017 at 6:55 pm

    Piga kaz kijana

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *