Cellebs

HISTORIA YA JUMA NATURE

on

Juma Nature ni mzaliwa wa jijini  Dar es salaam katika hospitali ya ocean road mwaka 1980.Jina lake halisi ni Juma Kassim Ally

Anasema kabla hajafikiria kuwa mwanamuziki alikuwa ni mchezaji mzuri wa soka katika timu za uswhilini maarufu kwa jina la ‘cha ndimu’
Anaeleza kuwa pamoja na kucheza soka katika timu ndogo wakati huo akisoma shule ya msingi Kurasini,alikuwa akiwaza kuwa kipaji hicho cha soka ndiyo ‘kingemtoa’ na kumsaidia maishani.
Anabainisha kuwa alisoma shule ya msingi kwa shida na baada ya kumaliza akuchaguliwa kuendelea na masomo ya sekondari.

“elimu ya ‘kibongo’ bili ya kuwa na mpango mbadala wa masomo ya ziada ni vigumu kufaulu. Wenzangu walikuwa na uwezo walisonga mbele mimi nikaishia hapo”,anasema Nature.
Anafafanua kuwa kutokana na familia yake kutokuwa na uwezo wa kumsomesha, binafsi alikuwa na moyo wa kusoma na aliazimia kufanya analoweza ili ajiunge na sekondari mwaka unaofuata baada ya kusota nyumbani kwa mwaka mmoja baada ya kumaliza elimu ya msingi.

“Nilikuwa naishi uswahilini,biashara ya kwanza wakati ule kwa watoto kama mimi,ilikuwa kuuza vyuma chakavu,hivyo nilikuwa kiguu na njia katafuta malighafi hiyo na kuuza,lengo ikiwa kutafuta ada”Alisema Nature
Msanii huyo nyota anasema kwamba alikuwa akiongeza kipato chake kwa kazi nyingine ikiwemo kupasua mawe eneo la Kurasini, kusukuma mikokoteni ya maji na mizigo,pia kuokota mkaa na kusaidia wazazi kuuza vitumbua.

“Baada ya kukusanya fedha hizo nilipata fedha ya kianzio za kulipia shule binafsi iliyopo maeneo ya Temeke(hakupenda kuitaja)”Anasema Nature
Anaeleza kuwa alisoma huku akifanya kazi hizo ili kujikimu katika mahitaji mbalimbali ya shule ikiwemo kulipia mitihani ya kila wiki,kununuia madaftari vitabu na vifaa vingine vya shule.

Nature anasema kuwa akiwa kidato cha tatu ndipo alipata hisia za kupenda muziki,ambapo walikuwa wakienda katika kumbi za starehe na kukutana na vijana aliokuwa wakiimba kutoka shule mbalimbali.
Anasimulia kuwa wakiwa shuleni,kulikuwa na mpango maalumu wa kupelekwa katika semina ili kujikinga na maradhi ya Ukimwi,matumizi ya pombe na dawa za kulevya.

Anafafanua kwamba walikuwa wakifanya uhamasishaji katika ukumbi wa Amana Center uliopo Ilala pamoja na ukumbi wa Ruaha Galaxy uliopo Kimara.
Anabainisha kwamba,hapo ndipo alianza kutunga mashairi akioanisha na kile walichokuwa wakifundishwa na kuimba peke yake akijikumbusha.”Hapo nilihisi kuna kitu kipo ndani yangu kuhusu muziki”.
Anasema hisia hizo ndizo zilimfanya awashawishi vijana wenzake watatu kuanzisha kikundi kilichokuwa kikijulikana kwa jina la For Skills Gangstar(FSG),ambalo kiongozi wake alikuwa ni yeye akitumia jina la Nature man.Anawataja wenzake hao kuwa ni Mark 2B,chrissna Dollo.

“Kama kuna watu niliokuwa nawakwaza wakati huo basi ni wazazi wangu.Walikuwa wanatiwa ndimu na majirani kuwa muziki ni uhuni,hivyo mimi nitapotea.Nyumbani moto ukawa ukiwaka kila niliporudi,hivyo nikiwa njiani kurudi, ninapanga maneno mazuri ya kumliwaza mama.Yaimtuliza jazba kwa siku husika na kupata chakula,siku nyingine kilikuwa kinawaka hata chakula nilinyimwa”.Anasema Nature.
Anaeleza kuwa wakiwa na kundi hilo walipata changamoto nyingi ikiwemo kutembea kwa miguu kwa umbali mrefu kutafuta shoo za kuimba ili watambulike.

“Tuliwahi kutambea kutoka Posta hadi Kimara mara ya kwanza tulisikia kuna shoo ya jamaa fulani, tukatoka Kurasini hadi Posta kumbe hatukusikia vizuri ilikuwa ni Kimara na tukalaimika kutembea hadi kimara kwa miguu”,Anasema
Anasimulia kuwa mwaka 1999, waliingia studio iliyokuwa chini ya mtayarishaji Endrico, inayoitwa Sound Craftaz na kurekodi wimbo wa kwanza alioupa jina la ‘Jambo hili ni batili’
Anaeleza kuwa mashairi ya wimbo huo yalikuwa yakilenga kupiga vita matumizi ya dawa za kulevya ambayo kwa wakati huo yalikuwa yameshamiri.

Anabainisha kuwa wimbo huo ulifanikiwa kusikika katika kituo cha redio one,akieleza kuwa kabla ya kupeleka studio kwa kuwa yeye ni kiongozi ailazimika kurui mtaani kuokota vyuma chakavu ili kupata fedha kununulia kanda ya kurekodi wimbo huo na kuziambaza studio.
Anafafanua kuwa iliwachukua mwezi mzima kutafuta sh:3,000 za kununulia kanda tupu

“Sikujali kuwa mimi ni kiongozi kwa kuwa niliokuwa nao kwenye kundi hawakuwa na uzoefu wa kuokota vyuma chakavu kama mimi.Nililazimika kuokota kwa kazi mbili,ada na kununulia kanda.

“Mwaka 2000 ni wa historia kwangu kwani nilihitimu kidato cha nne kwa shida na kufanikiwa kuupeleka redioni wimbo wetu tuliorekodi”,Anasema Nature
Hata hivyo anasema katikati ya mwaka 2000 kundi lao lilivunjika sababu ikiwa kila mmoja alitafuta njia yake kimaisha baada ya kumaliza shule
Nature anasema hali hiyo haikumkatisha tamaa na kutembea kwa miguu hadi Kimara kutafuta shoo za kuimba ili kujenga urafiki na wanamuziki wakubwa.

“Kipindi hicho nilidhailishwa sana na makondakta wa daladala.Kuna wakati nilichoka na kuamua kuvaa nguo za shule,nikajidi mwanafunzi huku nikionekana baba mzima.Nilishushwa njiani kwa kukosa nauli au kushindwa kuelewana na konda”Anasema Nature
Anaeleza kuwa kama ilivyo maisha ya uswahilini,majirani na watu wanaomfaamu walimwona kama chizi na kusema kwa maneno ya kejeli,wakimchukulia kuwa ni mwizi,mtukutu mvuta bangi na mambo yanayofanana na hayo ingawa ukweli hakuwa na sifa hata moja kati ya hizo.

“Kutoka kimuziki kilikula akili yangu yote wakati huo.Hata nilipoambiwa kuna shoo Kibaha,bila kualikwa na kuhisi naweza kupata nafasi ya kuimba hata wimbo wangu mmoja,ningeenda bila kujali kama nina nauli au sina.Hakuna mtu hata mmoja wa familia yetu ambaye ningemwambia anipe nauli niende huko na kukubali,waliona ni uhuni na upuuzi”.Alisema Sir Nature

 Mpenzi msomaji wa blog hii, kumbuka uonapo tangazo la bidhaa yeyoye hapa kwetu na ukanunua bidhaa hiyo, na mimi nitakua nmepewa kitu kidogo, hivyo utakua umenisidia, Ubarikiwe tena na tena

Amazon.in Widgets

Mtokambali 728x90

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *