Cellebs

Mfahamu mkufunzi mashughuri wa mpira Jose Mourinho “The Special One”

on

Jose Mario dos Santos Mourinho Felix amezaliwa tarehe 21 mwenzi wa kwanza mwaka kwanza mwaka 1963 katika mji wa Lisbon mtaa wa Setubal huko Ureno, ni mtoto wa Felix Mourinho na Maria. Baba alicheza mpira kisha baadaye alichukuwa mafunzo na kuwa kosha wa mpira wa miguu mama yake alikuwa mwalimu wa shule ya msingi. Akiwa china na miaka 18 baba yake alihama nyumbani hivyo Mourinho Alibaki na mama yake, mama alimwambia mwanae ajiunge na elimu ya chuo kikuu kwenda kusomea masomo ya biashara lakini Jose Mourinho aliacha chuo kwa sababu mpira ulikuwa upo kwenye damu.
Mourinho aliamua kumfuata baba yake katika miji ya Porto na Lisbon ambako baba yake alikuwa kocha katika timu ya Rio Ave ambapo alimwangalia baba yake akifundisha na kusikiliza mafunzo ya mpira yakitolewa na baba yake alihitimu mafunzo yake kisha alienda kusoma sayansi ya michezo katika ngazi ya stashahada kwa muda wa miaka 5 katika Technical University of Lisbon.
Katika miaka ya 1990’s alianza rasmi maswala ya kufindisha timu na alianza kufunisha klabu ya Victoria de Setubal kisha baaaye mwaka 1992 alipata nafasi ya kufanya kazi na Bobby Robson kama kocha msaidizi na mkalimani katika klabu ya Sporting Lisbon. Mwaka 1993 Bobby Robson alihamia klabu ya FC Porto na kumchukua Mourinho kuwa kama kocha msaidizi na mkalimani. Walifanikiwa kuchukua vikombe tofauti toufauti vitatu katika nchi ya Ureno na kuifikisha Nusu fainali timu ya Sporting Lisbon katika mashindano ya klabu bingwa Ulaya.
Mwaka 1993 Bobby Robson alihamia katika timu ya Barcelona akiambatana na Jose Mourinho ambaye alihama na familia yake kuelekea Hispani, baaada  ya Bobby Robson aliondoka Barcelona na Mourinho alianza kufanya kazi na Luiz Van Gaal kama kocha msaidizi pia Van Gaal alimruhusu Mourinho  kuongoza timu kwenye mashinano ya Copa Catalunya na kushinda ubingwa huo mwaka 2000 pia kukiongoza kikosi B cha timu ya Barca.Mwenzi wa 9 mwaka 2000 Benfica ilimuhitaji Jose Mourinho kuwa kama kocha msaidizi lakini alipomwambia Van Gaal alimjibu kama huendi kuwa kocha mkuu baki hapa lakini Jose aliamua kwenda kuwa kama kocha msaidizi katika timu ya Benfica lakini baada ya wiki nne tuu kocha mkuu aifukuzwa na Jose alipewa nafasi ya Kocha mkuu baada ya mienzi 4 tuu aliacha kazi katika timu ya Benfika kutoka na matatizo ya uongozi.
2002 alifundisha timu ya FC Porto kama kocha mkuu na kushinda mataji kama ubingwa wa ligi ya ureno msimu wa 2002-2003 pia aliifikisha fainali ya UEFA msimu huohuo, 2003-2004 alishinda mataji matatu ambayo ni ligi kuu ya ureno, UEFA super cap na ligi ya mabingwa Ulaya kwa kuifunga Monaco magoli 3 kwa sifuri. kisha baadaye mwaka 2004 alijiunga na timu ya Chelsea na kushinda
mataji  2004-2005 walichukua kombe la ligi kuu, Carling Cup, 2005/06 alishinda kombe la FA na ligi kuu,
2008 mwenzi wa sita alijiunga na Inter Millan na kuwapa ubingwa wa ligi ya mabingwa ulaya mwaka 2010 kisha akahamia Real Madrid mwaka 2010 mwenzi wa tano na kuwa ubingwa wa Copa del Rey, 2012 alishinda ubingwa wa ligi kuu hispania kisha 2014 Alirudi tena Chelsea ya kushinda Taji la ligi kuu na 2015 aliachana klabu baada mfulilizo wa matokeo mabaya na Kujiunga na timu ya Manchester United kwa mkataba wa miaka 3.
Ameshinda mataji 16 tofauti tofauti kwa muda wa miaka 17 kama kocha mkuu wa timu za Porto kashina 4 Chelsea 5 Inter Millan 4 na Real Madrid 3.
 
source. www.wikipedia.com
Mtokambali 728x90

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *