Cellebs

Mfahamu kiundani mwanadada Joketi Mwongelo

on

   Jokate Mwegelo  ni miongoni mwa vijana wa kitanzania wenye vipaji mbalimbali ambavyo wanavitumia ipasavyo. Mbali ya kujulikana zaidi kamamshindi namba mbili (2) wa shindano la kumsaka mrembo wa Tanzania mwaka 2006 na Balozi wa kinywaji cha Redds, Jokate pia ni mwanamitindo na msimamizi wa shughuli mbalimbali (MC). Isitoshe mwaka huu ameingia pia kwenye ulimwengu wa uigizaji filamu kama alivyoonekana katika filamu yaFake Pastors iliyoingia sokoni miezi michache iliyopita.
Kama hiyo haitoshi, Jokate pia ni mtengenezaji mzuri wa matangazo ya radio kwa kutumia sauti yake. Hivi karibuni tulipata nafasi ya kufanya naye mahojiano kuhusu mambo mbalimbali yakiwemo historia ya maisha yake, kazi zake, ushauri alionao kwa vijana wenzake nk.

Amezaliwa katika jiji la Washington DC huko marekani mwaka 1987 ambako huko ndio wazazi wake walikuwa wakifanya kazi. Walirudi Tanzania hapo Jokate alianza masomo yake katika shule ya Olympio Primary School na kwenda sekondari katika shule ya St. Antony’s high school alifaulu na kwenda A  LEVEL  katika shule ya Loyola High School  zote zipo Dar es salam kisha alifaulu na kwenda Chuo kikuu Dar es salam na kuchukua masomo ya Political Science.

Mwaka 2006 alijiingiza katika mashindano ya Ms Tanzania na kuwa mshindi wa pili wazazi wake hawakuchukulia vibaya walimsisitiza na kumwambia afanye yote lakini asisahau elimu. Watu ambao wamemhamasisha na kumpa hamasa ya kufanya kazi ni Mtanzania Irine Uwoya na Tyra Banks.

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *