Cellebs

Historia ya Hekima Raymond

on

 

Hekima Raymond mwaka 1980 katika nchi ya Tanzania mkoa wa Kilimanjaro wilaya ya Moshi vijijini katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC  baba yake ni mchaga na mama yake mnyakyusa mnamo mwaka 1991 baba yake alimnunulia kinanda baada ya kuona akipiga kinanda cha rafiki zake vizuri sana, alifanikiwa kupiga kinanda katika Band ya Mashirooms.

Mwaka 1993 alijiunga na St. Augustine Seminary School ndipo alianza kujifunza nota na ala za muziki, ambako alimpata rafiki yake mkubwa Bishop Mathias Isuja kwa kipindi hicho alikuwa mfupi kiasi kwamba hafiki chini kwenye kinanda akiwa akipiga kinanda katika kwaya ya St. Paul’s huko Dodoma.

Ilipofika mwaka 2005 alimaliza masomo yake katika Chuo kikuu cha Sokoine na kupata shahada ya Kilimo mwaka 20008 alitumbuiza katika kwaya za mozarts, handles messiah na Vivald akiambana na mpigana kinanda na mwongozaji wa kwaya kutoka Sweden anayeitwa Fabian Stevenson.

Aliendelea kujizolea umaarufu zaidi na zaidi kwa umahiri wake ambapo mwaka 2015 aliweza kutumbuiza katika Serena hoteli Tchaicovsty symphony numbari 5 katika kongamano lililohusisha viongozi wa siasa na wa dini mbalimbali pamoja na wafanya biashara maarufu kwa ajili ya kuomba uchaguzi wa amani.

Mwaka 2016 mwenzi wa 5 Hekima ameweza kupiga nyimbo ya kwaya ya kiswahi kwa kutumia Symphony namba 9 na kuwa kazi ya kwanza kutengenezwa katika nchi za Afrika mashariki na kati kusikika na kutengenezwa kwa lugha ya kiswahili. alichaguliwa kushiriki katika utumbuizaji katika tamasha la Social Change through the Arts by the US Department of State.

Hekima amechaguliwa kuwania tuzo ya Outlook Inspirational inayotolewa na kituo cha utangazaji cha Wingereza BBC akiwa anashindana na watu 50 katika kipengele hicho. tuzo hizi zitatolewa mwenzi wa 7 tarehe 4 mwaka 2016.

Sources;
www.hekimaraymond.com
www.TheCitizen Tanzania.com

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *