Cellebs

Ifahamu historia ya Chiristian Ronaldo aka CR7

on

 Amezaliwa Santo Antonio mama yake anaitwa Maria alikuwa mama ntilie na baba yake alikuwa akifanya kazi kama Gardener katika manispaa ya mji huo. Bibi yake asili yake ni visiwa vya Cape Verde huku Africa. Ronaldo Dosantos Aveiro amezaliwa mwaka 1985 tarehe 5 mwenzi wa nne katika familia ya watoto watatu.

Akiwa mdogo alikuwa akilala chumba kimoja na dada zake wawili kitu ambacho kilimuumiza sana. Akiwa na miaka 14 alimwambia mama yake kwamba anataka kucheza mpira kama kazi mama yake hakupingana na mawazo ya mwanaye hivyo alimruhusu CR7 kucheza mpira.

Akiwa na miaka kumi alijiunga na klabu ya Nacional baaadaye alijiunga tena na Sporting CP . Alipofikisha miaka 15  aligundulika ana matatizo ya moyo hivyo alifanyiwa upasuwaji na kufanyiwa matibabu na kumaliza salama matibabu yake.

Mwaka 2002 alifanyiwa jaribio katika klabu ya Arsenal pia mwaka huohuo alifanya jaribio katika klabu ya Liverpool kote makocha wa timu hizo walimuona CR7 kwamba ni mchezaji mzuri sana. Mwaka 2003 klabu na Man United ilicheza na Sporting CP na kufungwa mabao matatu huko Ureno baada ya mchezo wachezaji wa Man United walimzungumzia sana CR7 na kumwomba Furgason amsajili Ronaldo.

Mwaka 2003 CR7 alisajiwa rasmi na Man United kwa ada ya Euro milioni 12.4 na kukabidhiwa jezi namaba saba. Mwaka 2004 alishinda kombe la FA, mwaka 2007 na 2008 alipata tuzo ya mchezaji bora wa dunia. Ilipofika mwaka 2009 CR7 alihamia katika klabu ya Real Madrid kwa ada ya Euro milioni 94.

Akiwa huko aliweka rekord ya kufunga timu zote zinazoshiriki ligi ya LA liga pia msimu wa 2013 hadi 2014  aliibuka mfungaji bora wa UEFA pia ameweka Rekodi ya kufunga magoli 200 katika mechi 178 katika liga ya LA liga. Mwaka 2015 aliweka rekodi ya mfungaji bora wa muda wote UEFA baada ya kufunga magoli 82 pia aliweka rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa Real Madrid.

Katika timu ya taifa mwaka 2003 akiwa na miaka 18 alicheza mechi yake ya kwanza. Ameshiriki mashindano makubwa kama Euro 2004,2008 na 2012 pia kombe la dunia 2006,2010 na 2014 katika timu ya taifa yeye ni wa kwanza kufikisha magoli 50 pia ni mfunga bora wa muda wote wa mashindano ya kombe la ulaya amefunga magoli 113. Ronaldo amekuwa mufungaji bora wa UCL toka mwaka 2013 mpaka 2017 pia ameweza kuchukua kombe la Ligi ya mabingwa Ulaya mara mbili mfulilizo akiwa na real Madrid mwaka 2016 na 2017.

Mtokambali 728x90

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *