Cellebs

HISTORIA YA ALIKO DANGOTE

on

Ni mnaigeria ambaye anamiliki DANGOTE GROUP amezaliwa tarehe 10 mwenzi wa nne mwaka 1957. Kampuni ya Dangote Group inafanya kazi Nigeria, Benin, South Africa, Cameroon, Ghana, Togo, Tanzania na Zambia. Mwenzi wa kwanza  mwaka 2015 imekadiriwa anamiliki utajiri wa kiasi cha dola za kimarekani billion 18.6.Gazeti la Forbes imemuweka Dangote kama tajiri wa 67 Duniani na wakwanza Africa. Mwaka 2014 aliweza kufika nafasi ya 23 katika matajiri bora duniani.

ANAKOTOKA

Aliko Dangote anatoka ukoo wa Hausa  katika jamii ya Kano katika nchi ya Nigeria ametoka katika familia ya kitajiri ya kiisilamu. Dangote aliwahi kusema alipokuwa shule ya msingi alikuwa ananunua sukari na kuanza kuuza kwa hiyo alianza kupenda biashara toka utotoni.

BIASHARA YAKE


Dangote Group ilianzishwa mwaka 1977 kama kampuni ndogo. Ila kwa sasa inafanya kazi kaika nchi zaidi ya tano africa. Hii kampuni pia inasambaza sukari , vinywaji laini katika nchi ya Nigeria. Dangote wanamiliki asilimia 70 ya sukari ambayo inatumika katika nchi ya nigeria pia inazalisha tani 800000 za sukari kwa mwaka.

Mbali na apo wanahusika na uuzaji wa pamba saruji pia anamiliki viwanda vya kutengeza nguo katika nchi mbalimbali za Africa na pia anameajiri watu zaidi ya 11000 katika kampuni yake. Pia anamiliki kiwanda cha saruji katika nchi ya Tanzania

TUZO

Dangote was named as the Forbes Africa Person of the Year 2014.
Mtokambali 728x90

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *