Cellebs

Historia ya Akon

on

 

Aliaumie Damala Badara Akon Thiam ni Mwanamuziki, mwandishi wa nyimbo, mfanyabiashara, mtayarishaji wa muziki na muigizaji, amezaliwa tarehe 16 mwenzi wa 4 mwaka 1973 huko Senegal mtaa wa St. Luis baba na mama yake wote walikuwa wanamuziki akiwa na miaka 7 Akon alijifunza kupiga kinanda, gitaa, ngoma n.k zaidi ya vyombo tano vya muziki.Mwaka 2003 alifungwa jela miaka mitatu kutokana na swala ya kuhusishwa ya wizi baada ya kutoka alikutana na jamaa anayeitwa Stephen na ndiye mtu aliyegundua kipaji chake kisha walikuwa marafiki na jamaa huyu alimfundisha sana Akon maswala ya muziki akiwa huko Atlanta, Georgia huko Marekani alishindwa kusaini katika record label ya bwana Stephen hivyo akabaki mtaani tuu.

 

Mwaka 2004 Akon alitoa albamu yake ya kwanza inayoitwa Trouble ikiwa na nyimbo kama lock up, lonly, pot of gold na getto Lock up ilifika namba 8 katika chati za muziki mbalimbali ndani ya nchi za Marekani na Wingereza wakati  ilifika namba 5 Ghetto ilifanya vizuri sana katika redio  kwenye DJ Green Latern pale ilipochanganywa na nyimbo za 2pac na BIG. Mwaka 2005 alitoa nyimbo yake ya lonely ambayo ilifika namba tano katika chati ya Billbord top 100 pia katika nchi kama Wingereza, Australia na New zeland ilifika namba moja hivyo kumpa umaarufu sana hivyo kupata nafasi ya kushirikishwa katika Albamu ya Young Jeezy inayoitwa let it, thug motivation 101.

Mwaka 2006 chini ya usaidizi wa Interscope Record aliweza kuanzisha Record label yake inayoitwa Kon live distribution na kutoa albamu yake ya pili inayoitwa Convicted  albamu hii iliweza kufika namba 2 katika chati ya Billboard top 200 na kuuuza nakala zaidi ya 286000 kwa wiki moja. Ilipewa tuzo ya platnum baada ya wiki saba kisha triple platnum baada ya kuuza nakala milioni 3 nchini Marekani. alitoa albamu yake ya tatu inayoitwa freedom mwaka 2008. 2016 alitoa albamu ya 4 inayoitwa Stadium.

Jarida la Forbes lilisema utajiri wake ni  $13 million  2011, $21 million  2010, $20 million  2009 na $12 million  2008. anamiliki mgodi wa dhahabu huko Africa kusini pia mwaka 2014 alifanya kampeni yake ya Akon Lighting Africa ambayo alifunga umeme katika nchi15 za Africa,. amefanya filamu kama

  • Black November(2012)
  • American heist (2014)
  • Popstar; never stop never stop (2016)
Amefanya matamasha yafuatayo;-
  • Dar es salam, Tanzania One-off Concert (2006).
  • Tamasha la Konvicted  ( 2007na 2008)
  • Tamasha la Sweat Escape (2007)
  • Tamasha la Good Girl Gone Bad na Rihana ( 2008)
  • Konvict Muzik Tour na T-Pain (Australia only, October 26–27, 2009)
  • Summer Tour, (Brazil-leg only, January to February 2010)
  • OMG na Usher (North America Second Leg, April – June 2011)

 

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *