Cellebs

HISTORIA NA HARAKATI ZA KIMUZIKI ZA MSANII LINEX a.k.a SANDE MJEDA

on

Ameanza mwaka 1999  kwa kutungia wasanii nyimbo ambayo walifanya vizuri sana kipindi hicho ila hawakumtaja katika sehemu yeyote, aliumia sana kwa sababu aliona watu wakiweza kufanikiwa kimuziki kwa ajili ya uandishi wake. Aliacha kazi ya kuwatungia watu nyimbo na kuanza kuimba viitikio katika nyimbo za watu, Kwa siku aliweza kuimba viitikio 3 ambacho kila kimoja alilipwa 30,000.

Aliamua kuacha kuimba kwa mwaka mmja kisha akaanza kufanya mafunzo katika bendi alikuwa akienda kwenye mazoezi tuu lakini jukwaaani alikuwa hapandi kabisa hii ni kwa sababu hakupenda kujulikana kuwa yeye ni msanii kwa sababu alijua kwamba muda bado wa yeye kujutambuisha katika bongo fleva. Alianza kutafuta hela kwanza ndio akafanya muziki lipata kiu ya kurekodi sana lakini alikaza moyo ili afanya muziki vizuri.

Baada ya kufuatwa na mtu aliona muda wake umefika alitoa nyimbo ya “mama halima” nyimbo ambayo alitunga miaka miwili kabla yajaitambulisha katika hewani, Marafiki zake wengi waliachana naye baada ya kuona kwamba hapambani kuwa msanii mzuri,

Baada ya hapo Sande mjeda alifululiza kutoa nyimbo kali kila mwaka kisha aliweza kukaa kwenye chati za muziki wa bongo fleva. Anasema mtu ambaye amemuweka hapo alipo na anamheshimu sana ni producer anayeitwa prof. ludigo ndiye aliyebeba talent yake. Anasema kwamba Mungu amekupa kipaji ili utumie urudishe utukufu kwake.

 

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *