Health&Food

Haya ndiyo magonjwa yanayoweza kusababisha miguu na tumbo kuvimba

on


Ini kushindwa kufanya kazi

  • Hii husababisha sehemu ya tumbo kujaa maji na mtu kuonekana tumbo kuvimba hii ni kutokana na mshipa wa damu unaopeleka damu katika moyo kutoka kwenye ini kuathiriwa na kusababisha damu kwenda kwa taratibu hivyo madini ya kalishamu yaliyopo kwenye nyama za mwili hasahasa eneo la tumbo kunyonya maji yaliyopo ndani ya mshipa huu wa damu na kusababisha tumbo kuvimba.
 
Moyo kushindwa kufanya kazi
  • Hii husababisha Miguu na mikono kuvimba kisha mwili mzima kuvimba hii ni kutoka na moyo kutofanya kazi yake ya kawaida ya kupokea na kupeleka damu katika maeneo ya mbalimbali ya mwili hivyo kusababisha damu nyingi kutwama katika maeneo ya mwili kisha kujaa katika nyama za mwili.
Figo kushindwa kufanya kazi
  • Kazi kubwa ya figo ni kuhakikisha inaondoa sumu, madini na maji yaliyozidi katika mwii ili kuhakikisha kunakuwa na uwiano wa vitu hivi katika mwili wa binadamu sasa pale ambapo figo inashindwa kuchuja damu ambayo ni chafu iliyotoka katika maeneo mbalimbali ya mwili husababisha maji na madini hasahasa madini ya kalishamu kubaki katika mzunguko wa damu hivyo kupelekea wingi wa maji katika mwili pale ambapo yanakosa sehemu ya kwenda nyama za mwili huamua kuyachukua na kuyahifathi hivyo kusababisha mwili kuvimba.
Mtokambali 728x90

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *