Health&Food

Haya ndiyo madhara ambayo hutokea mwilini pale ambapo mtu anashindwa kuwahi tiba ya ugonjwa wa malaria.

on

1. Huaribu ubongo ; Vijidudu vinavyo sababisha malaria huingia katika damu na kufika katika eneo la ubongo na kusababisha mtu kuwa na dalili zifuatazo kuchanganyikiwa, doti doti za damu kuonekana katika macho, mgonjwa kutokuwa na fahamu na mwili wake kukakamaa pia kupata degedege.  N.B mgonwa huwa hapati dalili zinazofanana na zile za homa ya uti wa ugongo.

2.Upungufu wa damu mwilini ; Viidudu vinavyosababisha malaria huingia katika mfumo wa damu kisha kuanza kushambulia chembe chembe nyekundu za damu hivyo kuziua kisha kusabbabisha wingi wa damu wa binanadamu kushuka dalili zake ni kama kizunguzungu, viganja vya mikono kuwa vyeupe zaidi, kichwa kuuma sana na mkojo kutoka ukichanganyikana na damu.

3. Upungufu wa sukari mwilini ; kutokana na malaria kusababisha joto la mwii kupanda sana hupelekea pia sukari ya mwilini kushuka pia uhitaji  mkubwa wa chakula wa vijidudu vinavyosababisha malaria hutumia sukari hivyo hupelekea pia sukari kupungua mwilini.

4.  Figo kushindwa kufanya kazi ; malaria husambulia figo katika sehemu mbalimbalii  hivyo kupelekea figo kushindwa kuchuja damu vyema na kusababisha sumu kuzunguka ndani ya mwili pia dallili ambazo huonekana kwa mgonjwa ni kutokupata mkojo kabisa au kupata mkojo mdogo sana pia baadhi ya sehemu za mwili kujaa maji.

5. Ini kushindwa kufanya kazi ; Vijidudu hivi hushambulia pia ini hivyo kusababisha kushindwa kuchuja sumu inayoingia mwilini iliyobebwa na vyakula pamoja na damu chafu mgojwa huonekana ana kuwa na rangi ya manjano katika maneo ya kiganjani, kwenye kucha, na kwenye macho.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *