Uncategorized

HAWA NDIYO WATAYARISHAJI MUZIKI( PRODUCERS) BORA TANZANIA

on

P FUNK MAJANIHuyu ni mmliki wa BONGO RECORDS ndiye mwanzilishi wa muziki wa kizazi kipya yaani Bongo fleva hapa Tanzania. Amesomea degree ya sound engineering. Amefanya kazi na wasanii wakubwa Bongo kama vile Prof Jay, Sugu, Jay Mo, Juma nature na wengine kibao hapa bongo. Alianza hizi harakati za muziki mwaka 1992. kwa sasa hafanyi tena music kwa sasa.

Master Jay

Huyu ni mmiliki wa MJ RECORD alianza harakati zake za muziki hapa Bongo baada ya kumaliza degree yake ya sound engineering huko marekani amenya nyimbo nyingi sana hapa bongo na wasanii kama mwana fa, A.Y, Feruz, na wengine wengi.

Marho Chali

Alianzia kazi yake katika studio ya KAMA KAWA RECORDS alifanya nyimbo kibao bora pale kama kawa na baada ya hapo Master Jay alimchukua na kumpeleka katika studio yake ya MJ RECORDS na kutengeneza nyimbo kali nyingi hapa Tanzania. Ni producer ambaye ni mbunifu sana kwa sasa hapa Bongo na kupewa jina la Dr. Macho Chali.

Nah reel

Ni producer ambaye anamiliki studio yake ya THE INDUSTRY, amefanya ngoma kali hapa africa ambazo zimechukua headlines katika bara la Africa, Ameweza kuweka nyimbo Tano katika top ten za MTV DASE AFRICA NA TRACE TV  ambazo ni Game,Nana, Olele, Looking for you na Never ever ya V Money. alianza kutengeneza mziki akiwa kama kawa records baadaye home town records

ndiyo akaanzisha studio yake.

Man Water 

Anafanya katika studio zake za COMBINATION SOUND  alifahamika sana baada ya kutengeneza nyimbo za 20% ambazo zilimpa tuzo tano pia anafanya nyimbo na wasanii wa gospo nchini kama Bonnie Mwaitege. na wengineo.

Mtokambali 728x90

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *