Uncategorized

HAWA NDIYO WASANII WA BONGO HIPHOP WANAO NA WALIO ANDIKA MISTARI MIKALI ZAIDI

on

1. Mr II 

Mwanaharakati Huyu ndiye mwasisi wa bongo fleva na Hiphop bongo ana Albamu 12 ambazo hakuna msanii mwingine wa Hiphop anaweza kufikia. Nyimbo kama Mchaka mchaka, Kiburi, na nyingine kibao nyingi. yeye aliwatetea wamachinga sana katika maisha.
2. Prof jay
Huyu ni msanii ambaye amewasaidia sana vijana wangine kupata hamasa katika shughuli za muziki pia ni msanii ambaye ameweza kuwashawishi wazazi kuruhusu watoto wao kufanya muziki. Ametoa ngoma kama Ndio mzee, zali la mentali, Bongo dar es salam pia chemsha bongo. Nyimbo nyingi zake zimewaelimisha sana mavijanaa.
3. Afande Sele
Huyu ndiye msanii peke ambaye amepokea tuzo ya mfalme wa rymes ambayo hakuna msanii mwingine amewahi kupewa hiyo tuzo hiyo ambayo alipewa gari na Rais mstaafu  Mkapa. Ametoa nyimbo kama mtazamo, heshima n.k 
4. Mwana FA
huyu ni msanii ambaye anaamika kwa kuimba kiswahili sanifu na kujizolea umarufu hadi kujulikana kama mwana falsafa. Ametunga ngoma kama binabu, unanijua unanisikia, Alikufa kwa ngoma na ingekuwa vipi.
5. Fid Q
huyu ni msanii ambaye nyimbo zake na utunzi wake unakuwa mgumu kuelewa kwa sababu ya kutumia mafumbo nahau na misemo migumo ya kiswahili na hivyo kufanya nyimbo zake zisichokwe. Ametunga nyimbo kama Mwanza mwanza, propaganda, fid q dot com, chagua moja n,k.
6.Joh makini
huyu ni msani ambaye amepambana sana na kuonyesha roho ya kutokata tamaa na muziki anajulikana kwa tungo zake kali kama stimu zimelipiwa, wameinama, mfalme, chochote popote, n.k
7.J mo
huyu ni msanii ambaye hawahi kuchukua tuzo lakini ni mkali katika uandishi ameandika nyimbo kama maisha ya bodi, mvua na jua, tingisha n.k
8.A.Y
huyu ni msanii wa kwanza kufanya ngoma za kimataifa kwa wingi sana. pia ametoa ngoma kali kama usijaribu, usije mjini, raha tuu na nyingine nyingi.
Mtokambali 728x90

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *