LifeStyle

Hatua tatu za kujifunza kuwa na Hisia Akili ( emotional intelligent) zaidi.

on

Hisia  akili (Emotional Intelligent); huu ni uwezo wa kufuatilia mawazo yako na mawazo ya wengine, kuyatenga na ya wengine na kutumia taarifa za mawazo hayo kukuelekeza katika kufikiri na kutenda. 


1. Mafunzo makini ( attention training )

Umakini ni kila kitu kwa mtu mwenye utambuzi mkubwa na uwezo hisia. Maana yake ni kutengeneza akili ambayo ni tulivu na makini katika kuwaza kisha kupambanua fikra za wengine zinazoendana na hilo wazo ambalo akili imeliwaza yenyewe mwishoni kutoa jibu moja, Mafunzo makini ndio kiini cha HISIA AKILI.

2. Maarifa binafsi ( self  knowledge )

Kutumia umakini wako mwenyewe kufanya azimio la mtazamo wako kwa kutumia mfumo wako wa utambuzi na hisia, kwa kufanya hivi unaweza kuona fikra zako na mfumo wa hisia zako kwa uwazi sana.

3. Tengeneza tabia ya kutanguliza jamii katika akili ( create pro-social mental habits )

Kuwa na utu, heshima, busara na jitahidi kufanya mambo ambayo yanapunguza huzuni au hasira kwa mtu, watu au kikundi cha watu vivyo hivyo jitahidi kuongeza ufanyaji wa mambo ambayo yanaongeza furaha, upendo na amani kwa mtu, watu na jamii inayokuzunguka.

Mtokambali 728x90

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *