LifeStyle

Hatua 4 ambazo ukizifuata utapiga hatua kubwa katika uingizaji wa kipato

on

 

1. Hakikisha unaweka akiba ya asilimia 10% katika kipato chako

Haijalishi kipato chako ni shiing ngap wewe unachotakiwa ni kuweka tuu akiba mfano unapata kila wiki shilling elfu 3000 kama faida katika kazi yako kwa hiyo akiba yako ni 450 kila wiki mara nne ni 1800 kila mwenzi mara 12 ni sawa na elfu 21,600
hiki ni kiasi kidogo sana ambacho umeona jinsi baada ya muda kinavyoweza kuongezeeka na kuzaa kikubwa. achana na mambo ya dharura sijui harusi, epuka kutumia hela ya akiba kwa matumizi yako eti kwa malengo ya kulipa.

2. Hakikisha matumizi yako hayazidi kipato chako.

Katika kitu ambacho kinafanya watu waharibu kipato chao ni kukubali kubadishwa na pesa yaani na maanisha kuongeza matunuzi pale ambapo kipato kinaongezeka. acha kabisa huo ni ulimbukeni na kukubali kifikra na kimatendo kwamba maisha ninayoishi hayaendani na kipato ninachofanya hiyo haifai kamwe.

3. Zidisha dhahabu yako yaani wekeza

Kama wewe ni mwajiriwa tambua kwamba itafika mahali ambapo wewe hutoweza kufanya kazi za watu ipasavyo hivyo utastaafishwa kazi sasa ni muhimu wewe kuanza kujiwekeza toka mwanzo ukianza kazi kwa kutumia zile akiba zako asilimia 10% kwa ajili ya kujiajiri.

Pia kama wewe ni mjasiriamalli hakikisha unamtengeneza mtu ambaye atakuja kuendesha kampuni yako usiwe mchoyo jaribu kumpa kazi mtu ambaye unajua utamkabidhi uongozi mwandae hii itakufanya kampuni yako isishuke.

4. Penda kujisomea mwenyewe

Achana na habari za kuchati na kuongea na simu kuwa na utamaduni wa kusoma vitabu au kusikiliza vitu ambavyo vinakujenga katika muendelezo wa malengo yako. Inasekana asilimia 80% ya matajiri huwa wanapenda kutumia muda wao kusoma vitabu.

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *