Health&Food

Hatua nne za umwaaji na usaambaaji wa ugonjwa wa saratani

on

 

Hatua ya 0

saratani inaingia kazi “carcinoma in situ” Katika hatua hii seli za saratani huwa katika eneo la juu la sehemu ambayo mwili umeshambuliwa mfano ini, koo, mlango wa uzazi n.k. Katika hatua hii unaweza kupata matibabu na uwezekano wa kupona ni mkubwa.

Hatua ya 1

Katika hatua hii Seli za saratani zinaanza kushambulia sehemu ya mwili ambapo zimejitokeza mfano hupenya ndani ya nyama za koo au ndani kwenye mapafu ila hazijafika ndani kabisa huweza kuonekana kwa kipimo cha darubini.

Hatua ya 2

Katika hatua hii saratani imeshafika ndani ya eneo ambalo imelishambulia pia seli za saratani huanza kuenea katika sehemu za mwili ambazo zipo karibu na eneo lililoshambuliwa mfano kama kansa ya mlango wa uzazi hapa uwa imeanza kuenea katika sehemu za kizazi na uke.

3. Hatua ya 3.

Katika hatua hii hushambulia zaidi sana maeneo mengine yaliyokaribu na sehemu iliyoathiriwa mfano kama kansa ya koo hufika hadi tumboni, kwenye kinywa hadi katika koo la hewa.

Hatua ya 4

Katika hatua hii eneo ambalo limeshambuliwa huwa tayari limeshaaharibika kabisa kisha seli za saratani zinaanga kushambulia yale maeneo muhimu ya mwili kama moyo, figo, mapafu na ini.

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *