Cellebs

Mfahamu Producer Maxmizer na harakati zake za kimuziki

on

Jina lake la passport ni Shukuru Frank alianza kazi za kutayarisha muziki mwaka 2012 katika studio ya mazuu alifanya kazi hapo kwa muda wa miaka miwili kisha mwaka 2015  alihamia katika studio ya wakazi kwanza iliyopo chini ya kaka yake na msanii Chemical.

Ametengeneza nyimbo kama Pacha wangu ya Rich mavoko, Siri ya Barnaba na Vannesa, Q chief ya mdogo mdogo, Chemical Sielewi na VIP pia Aiyola ya msanii ambaye yupo chini ya lebo ya wasafi Harmonize.

Baada ya nyimbo ya Harmonize kufanya vizuri Africa msanii Olamide aliona hiyo nyimbo kisha akapenda midundo yake na kuamua kutafuta producer ambaye amefanya kazi hiyo. Olamide alimtafuta kupita Instagram kisha baadaye aliomba Maximizer amtumie E mail yake ili wawasiliane zaidi. Maximizer alimtumia nyimbo nyingine alizofanya kupitia email ya ofisi Maximizer anasema kwamba wamepanga kufanya kazi na hii itamfanya producer huyu kupenya kimataifa.

Mtokambali 728x90

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *