Cellebs

Mfahamu msanii kutoka Nigeria Davido kiundani zaidi

on

 

David Adedeji Adeleke(alizaliwa November 21 1992) anajulikana zaidi kwa jina la kisanii Davido,ni msanii,mwimbaji, na muandaaji wa njimbo pia ni raia wa Nigeria aliye zaliwa Marekani.Wimbo wake wa mwaka 2011 “Dami Duro” ulipokelewa vizuri ndani na nje ya Nigeria.Pamoja na kaka yake Adewale Adeleke, Davido ni mmoja wa wamiliki wa record label ya HKN Music(yenye wasanii kama Sina Rambo, B.Red na Deekay). Ameandaa nyimbo za wasanii kadhaa kama Naeto C, Skales, Tiwa Savage, na Sauce Kid.April 2012, ali saini mkataba wa usimamizi na MTN. Davido alishinda BET Award, Kora Award, Chanel O Music Video Award, Ghana Music Award, Nigeria Music Video Award, tuzo mbili za MTV Africa Music Award,tuzo mbili za African Music Magazine Award, tuzo tano za The Headies Award, tuzo saba za Nigerian Entertainment Award na tuzo mbili za Dynamix All Youth Award kati ya nyingine nyingi.

Davido alizaliwa Atlanta, Georgia na kupelekwa kuishi Lagos akiwa mdogo. Alitoa albamu ya “Omo Baba Olowo” mwaka 2012 yenye nyimbo kama “Back when” aliyomshirikisha Naeto C, “Dami Duro”, “All of You”, “Overseas”, aliyo mshirikisha Sina Rambo, “Ekuro”, “Gbon Gbon” pamoja na “Feel Alright” aliyo mshirikisha Ice Prince. Davido alitoa singles kama “Gobe”, “One of Kind”, “Skelewu”, “Aye”, Tchelete(Goodlife)”, “Naught”, pamoja na “Owo Ni Koko” zilizo kuwa kwenye albamu iliyokuwa itoke mwishoni mwa mwaka 2014. Kwenye mahojiano yake na Nigerian Tribune, Davido alisema kwamba albamu yake ya pili haitatoka mwaka 2014.

Januari 2016 Davido alitangaza kupitia Twitter kwamba amesaini mkataba na kampuni ya Sony BMG; tangazo ambalo lilikutana na matukio mchangnyiko.

MAISHA NA KAZI YAKE YA MZIKI
1992-2010:Maisha ya ujana na mwanzo wa kazi ya mziki.
Davido alizaliwa November 21, 1992 kwenye ukoo wa chifu Deji na Vero Adeleki huko Antlanta, Georgia. Baba yake ni mfanyabiashara wa Kinigeria wakati Marehemu Mama yake alikuwa ni mkufunzi wa chuo kikuu. Davido alisoma katika shule ya British International School iliyopo Lagos. Davido alisomea Biashara chu kikuu cha Oakwood University wakati akia Nigeria. Davido alianza kupenda mziki wakati akiwa Oakwood University. Alileta vifaavya mziki na kuanza kutengeneza midundo na kurekodi sauti. Aliondoka chuo kikuu cha Oakwood baada ya kuanza kupata alama mbaya za ufaulu na kenda kuishi London Uingereza, huko alijikita zaidi kwenya kurekodi na kuandaa nyimbo. Aliporudi Nigeria mwaka 2011 kazi yake ya muziki ilikuwa kwenye akili yake baada ya kukubali kujiunga na chuo kikuu cha Babcock University.July 2015 Davido alipata digrii ya muziki kwenye chuo kikuu cha Babcock.

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *