Health&Food

HALI UTE WA MLANGO WA UZAZI KABLA NA WAKATI WA HEDHI( yai kupevuka)

on

 

Ute wa mlango wa uzazi hubadilika kulingana na mwanamke yupo katika hali gani katika mfumo wake wa uzazi( reproductive system), Hii hufanyika ili kuweza kuruhusu wakati muda wa kuruhusu mimba kutungwa ute habadilika ili kuhakikisha kwamba ,mbegu za mwanaume zinaweza kwenda kwa kasi na kulifikia yai. Hivyo basi ni muhimu kujua hili kama mwananke kwa ajili ya kujilinda dhidi ya mimba usiyoitarajia;

HALI YA UTE.

  • Ute ukiwa mkavu au unanata; aina ya ute kama huu hauruhusu mbegu za kiume kusafiri na kuingia katika kizazi hivyo mimba haiwezi kutungwa hapa, Huu ute huwepo kindi mwanamke akiwa hayupo katika kipindi cha joto au kipindi ambacho yai bado halijapevuka.
  • Ute ukiwa na Rangi ya Cream(krimu) hapo mwanamke anakaribia kuingia katika kipindi cha joto pia yai linakaribia kupevuka bado hawezi kupata mimba.
  • Ute ukiwa kama majimaji au unyevu unyevu huu unaweza kusafirisha mbegu hadi katika kizazi na kama imebaki siku mbili au tatu yai kupevuka ukifanya tendo la ndoa hapa asilimia chache sana za kutapata mimba kwa sababu yai likipevuka litakutaana na mbegu ndani ya kizazi hivyo mimba itatungwa.
  • Ute ukiwa na rangi nyeupe kama yai libichi; ute ukiwa katika hali hii ndio mzuri kwa kusafirisha mbegu za kiume, pia hapa mwanamke ameshafika katika kipindi cha joto hapa tendo la ndoa likifanyika mimba inapatikana kwa asilimia zote.

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *