Health&Food

Fahamu maana,dalili na matibabu ya ugonjwa wa Upele.

on

Upele ni ugonjwa wa ngozi ambao  huwa na tabia ya mtu kuwashwa sana miwasho hii ikiwa imesababishwa na vimelea aina ya Mite sarcoptes scabiei. Ugonjwa huu huambukizwa kwa njia ya kugusana moja kwa moja na mgonjwa ambaye ameathiriwa na ukurutu pia unaweza kuambukizwa ugonjwa huu kwa njia ya kugusa kitu au vitu ambavyo vimeshatumiwa na mtu mwenye ukurutu mfano nguo na mashuka.

Ugonjwa huu hupenda kujitokeza sana kwenye maeneo yafuatayo kwenye mwili wa binadamu;-

 • makalio
 • mapaja
 • Sehemu za nje za uke au uume
 • kwenye kikwapa
 • kwenye chuchu
 • kisugudi

Dalili za ugonjwa huu wa Upele

 • kujikuna sana
 • kuwashwa sana

matibabu yake

 • oga mara kwa mara kwa kutumia sabuni ya Benzyl benzoate emulsion (BBE) hii hutumika wakati ukioga na maji ya uvuguvugu kisha baada ya masaa 24.
 • hakikisha unawatibu watu wote waliopo karibu na mgonjwa ili kuepusha ugonjwa kujirudia tena.
 • ili kutibu miwasho tumia Calamine lotion.

Njia za kujikinga;-

 • Oga mara kwa mara
 • Fua nguo zako kila mara
 • wapime na watibu au wapeleke hosipitali majirani, ndugu au jamaa ambaye anaugua ugonjwa huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *