Health&Food

Fahamu maana, dalili na matibabu ya ugonjwa wa Kisonono

on

Kisonono ni ugonjwa wa zinaa ambao huambukizwa na bacteria au kimelea kinachoitwa Nesseria Gonorrheae, Vijidudu hivi hupenda kushambulia sehemu za mwili zenye hali ya unyevuunyevu au umajimaji sehemu hizo ni kama vile;-

 1. Njia ya kutolea mkojo(urethra)
 2. Puru
 3. Uke
 4. Shingo ya kizazi.
 5. Macho

Ugonjwa huambukiwa kwa njia ya kujamiana, kunyonyana denda pia kufanya mapenzi kinyume na maumbile vyote bila kutumia kinga na mtu( mwanaume au mwanamke) ambaye ameathiriwa na ugonjwa huu. Watu ambao wana wapenzi wengi au wanaofanya mapenzi au ngono bila kutumia kondomu hawa wanauwezekano mkubwa kupata ugonjwa huu pia watu ambao wanatabia za kutumia madawa ya kulevya na ulevi.

Dalili zake hujitokeza baada ya wiki 2 hadi 14 baada ya mtu kuambukizwa, watu wengine hawaonyeshi dalili hizi moja kwa moja hii haiwazuii kuwaambukiza wengine huendelea kuwaambukiza wengine. Dalili zake ni kama zifuatazo:-

kwa wanaume

 • Kukojoa mara kwa mara
 • Uume kutoa matone matone yanayofanana na usaha
 • kupata vidonda kwenye koo la hewa
 • Mapumbu kuvimba
 • Kuvimba au kuwa na wekundu katika eneo la mbele la uume.

Kwa wanawake

 • Kukojoa mara kwa mara.
 • Uke kutoa umaji umaji mara kwa mara.
 • maumivu au kuhisi moto unawaka sehemu ya uke wakati wa kukojoa.
 • kusikia maumivu makali chini ya kitovu.
 • homa.
 • kupata vidonda katika koo la hewa.
 • damu za hedhi kutoka muda mrefu.
 • Kusikia mauvimu wakati wa kufanya ngono.

Damu na majimaji yaliyopo katika sehemu za puru,uume na uke huchukuliwa kwa ajili ya vipimo ili kutambua mtu kama ana ugonjwa wa kisonono.

Matibabu;-

 • Dawa ambazo hutumika kutibu ugonjwa huu ni pamoja na antbiotics kama vile Ceftriaxone ambayo hupewa mara moja kwa siku au mara mbili kwa siku kwa muda wa mwenzi au wiki dozi inategemea na mgonjwa alivyozidiwa, dawa nyingine ni Azithromycin.
 • Pia unaweza kupewa dawa za maumivu au za kupunguza joto kulingana na dalili zinazojitokeza.

 

Mtokambali 728x90

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *