Cellebs

Fahamu historia ya msanii kutoka Nigeria Patoranking

on

Patrick Nnaemeka Okorie amezaliwa tarehe 17 mwenzi wa tano mwaka 1990 amelelewa katika mji wa Ijegum huko Nigeria kisha baadaye alihamia katika mji mwingine unaoitwa Ebutte Metta alisoma katika chuo cha Citizen Comprehensive Collage pamoja na shule ya Jibrii Martin memorial school.Jina lake la kimuziki alipewa na jamaa mmja mjini lagos nchini Nigeria baada ya kuona jamaa anaweza sana kuimba na kucheza mziki wa Rege, wasanii ambayo anawapenda na waliomfanya mpaka kuingia katika muziki ni Chaka Demus, Luck Dube na Bob Marley.

Mwaka 2013 msanii Patoranking alitoa kibao chake cha kwanza kinachokwenda kwa jina la “Alubarika” ikiwa na maana ya “Baraka za Mungu” nyimbo ndio iliweza kumtambulisha katika sanaa ndani na nje ya Nigeria, Alubarika alimshirikisha msanii “Timaya” ambaye alikuwa anamsimamia katika record lebal yake inaypitwa Dem mama records. 2014 Patoranking alihama katika record lebal ya Dem mama iliyopo chini ya Timaya kisha kusaini kandarasi mpya na Foston Musik. Timaya alikaririwa akisema kwamba hakuwa na mkataba na Patoranking.

Mwaka 2014 mwenzi wa nne Patoranking alitoa nyimbo yake inayoitwa Girl “O” ambayo video yake aliifanyia London na muongozaji wa video maarufu huko Nigeria Mao Musa, mwenzi watano mwaka huohuo Msanii Tiwa Savage aliomba kufanya remix ya nyimbo hiyo Girl “O” remix ilifanyika na iliweza kushika namba 9 katika chart za MTV Base Naija top 10. 2015  ulikuwa mwaka mzuri kwa msanii Patoranking baada ya kutoa ngoma mbili kali ambazo ni Daniella na My woman My everything nyimbo hizi zote ziliweza kufika chart za juu kabisa katika MTV Base Naija top 10, Daniela iliweza kushika namba moja na My woman,My everything ikishika namba 2. Mwaka 2016 Patoranking aliweza kuteuliwa kama jaji wa mashindano ya kuimba huko Nogeria yaliyoitwa “The voice of Nigeria” na Albamu yake ya “God Over Everything” ambayo aliwashirikisha wasanii kama Sarkodie, Wizkid, Elephant Man na Pyno. Albamu yake iliweza kushika namba nne katika chart ya Billiboard top regge album.

Ameshinda tuzo 11  kati ya 27  alizoshiriki.

 

 

Mtokambali 728x90

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *