LifeStyle

Aya 3 muhimu ambazo kijana mpambanaji unatakiwa kuzisoma

on

 

Habari zenu mabibi na mabwana kaka zangu na dada zangu pia wadogo zangu natumaini mpo pouwaa, Pia mnaendelea vizuri kiafya na kimaisha kwa wale wanaumwa napenda kuwapa pole. Leo hii nimeamua kuwaandikia hii makala. Tafadhali naomba chukua dakika tano tuu na baada ya dakika tano utaona utofauti katika kitu ambacho ulikuwa unakiwaza.

Kijana mpambanaji pale ambapo unaona changamoto zinakuja katika maisha yako ndio muda ambao wewe unaanzakukua katika kitu ambacho changamoto hiyo imejitokeza chakufanya ni kwamba Kaa chini, Muite Mungu kisha tumia akili ambayo Mungu amekujalia kuchanganua njia za kutatua changamoto hiyo ( ukitumia hii kanuni basi changamoto yako utakuwa umeipatia suluhisho)


Kijana mpambaji unakosea pale ambapo unapata changamoto fulani ya kimaisha na kukimbilia vitu ambavyo vitatakufariji katika hali uliyonayo mfano pombe, kupiga stori na kuwa na mahusiano ovyo ya kimapenzi kwa pamoja hivi vitatu huwa havikupi suluhisho katika changamoto uliyonayo kwani pale ambapo utamaliza muda wa kutumia hivi vitu tuu tayari changamoto inarudi palepele cha msingi ni kukaa mbali navyo kwanza.

Kijana mpambanaji baada ya kuchanganua na kutengeneza suluhisho kisha kuona halitoshi kusuluhisha changamoto yako cha kufanya ni hiki “Tafuta mtu ambaye anaendana na malengo yako ambaye amebobea katika kitu unachokifanya ili akushauri kitu au mbinu ambayo inaweza kujazia kitu katika suluhisho lako ONYO epuka maneno ya watu ambao wanapinga na hawakusaidii katika lengo lako”


TAMBUA KWAMBA MAWAZO YAKO NI MAFANIKIO YAKO KWA HIYO TUMIA UBONGO WAKO KUTENGENEZA MAWAZO CHANYA NA KISHA JENGA IMANI YA KUYAAMINI MAWAZO YAKO

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *