Uncategorized

JE UNAJUA KWAMBA MSECHU AMEWAHI KUWA WA MWISHO DARASANI? SOMA HAPA

on


Amewahi kuzomewa jukwaani kwa sababu ya watu kuona haimbi vizuri na myimbo zake hazipokelewi na mashabiki pale anapotaka kuwaimbisha hii ilimsababisha yeye kuamua kurudisha hele ya shoo aliyopewa.

Amezaliwa katika mkoa wa Kigoma ni mtoto wa pili katika familia ya watoto wanne. Amesoma shule ya msingi Katumba na kujiunga na Shule ya sekondari ya Uchamma Tabora na kupata Daraja la 3 na kujiunga na Galanosi sekondari kombi ya EGM.

Akiwa galanosi sekondari allionekana kijana ambaye hana akili alikuwa akishika nafasi ya mwisho darasani na pia amewahi kuchapwa na mwalimu na kupewa zawadi za waliofaulu ili awakabithi wao mbele ya paredi.

Akiwa katika mtihani wa Uchumi aliufanya kwa nusu saa baada ya kuona kwamba atachelewa kwenda kwenye mashindano ya Bongo Star Search. Alipanda gari la AIR bus na kuelekea Kigoma Tayari kwa usahisi. Alishinda katika usaili kigoma na kuelekea Dar es salam.

2009 Alikuwa mshindi wa pili na Master J kumsaini MJ Records na kufanya ngoma yake ya hasira hasara,
katika ile milioni tano alimpa baba milioni 4 na alianza kupanga na maisha yalikuwa magumu sana. 

2010 Mke wake alimtia hamasa na kusihi akashiriki katika shindano la Tusker project fame na katika audition alifanikiwa kupita kwenda kuiwakilisha Tanzania huko Kenya. Wakati wa kwenda ilibidi adanganye kwamba baba anaumwa baada ya kuchelewa kwenda uwanja wa ndege, Hii ni kwasababu ya wanakwaya kumuitaji katika tamasha kama mwalimu wa kwaya.

Akiwa nafasi ya tano alipata habari kwamba amechaguliwa kujiunga na chuo kikuuu cha Dar es salam lakini alishindwa kwenda kwa sababu ya mashindano, Pia ilipofika mwaka 2011 shindano TUSKER ALL STARS lili anzishwa na Petter msechu alienda kushiriki akiwa huko pia alipigiwa simu na chuo cha uhasubu arusha IAA na kushindwa tena kujiunga kutokana na mashindano.

Alianza muziki katika kikundi cha  THE FOLLOWERS ambacho kilikuwa kinaimba nyimbo za kidini   na kutoa Albamu moja lakini walishindwa kuendelea kama kundi baada ya kutkuona maslahi na kile kikundi kilivyinjika na kila mtu kuamua kufanya mambo yake.

Katika kipidi cha kampani nyimbo yake ya Nyota ilimuingizia sana mkwanja hii ni kwa sababu ya waheshimiwa wengi na wabunge wengi kutaka kupatiwa nyimbo hiyo kama nyimbo ya kuwanadi katika kampeni zao. Alikuwa akichaji kiasi cha laki tano kama kima cha chini na Aliwafanyia wabunge zaidi ya 64.

Rude,Barnaba, Master J ni baadhi ya watu waliomwambia Petter Msechu kwamba hajui kutunga mashairi hii alimfanya ajikubali kuanza kuchukua jukumu la kutafuta mtu wa kumtungia mashairi hivyo aliongea na Barnaba na watunzi wengine maarufu hapa bongo ili aweze kusaidika na hiyoishu.

Mtokambali 728x90

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *