Cellebs

HISTORIA YA LIL WYNE

on

 

 

Alizaliwa kama Dwayne Michael Carter, Jr. na kukulia mjini Hollygrove karibu kidogo na mji wa New Orleans, Louisiana. Akiwa na umri wa miaka kumi na moja, akakutana na Bryan Williams, rapa na ndiyo mmiliki wa studio ya Cash Money Records. Baada ya makutano hayo, Wayne akarekodi rap flani ya michano katika studio hiyo ya Williams kwa kutumia chombo maalum cha kuweza kukujibu wakati unachana. Na kwa bahati nzuri michano hiyo ilimwacha hoi mmiliki huyo wa studio na kuthubutu hata kumwingiza Wayne katika studio yake. Wayne pia ana mtoto wa kike mmoja aitwaye Reginae Carter, aliyezaa na Bi. Antonia “Toya” Johnson, demu wake wa kitambo toka shule. Wawili hao walikuja kuoana wakati ule wa Siku Kuu ya Wapendanao ya mwaka wa 2004, lakini wawili hao walikuja kutarikiana mnamo mwaka wa 2006.

Dwayne Michael Carter, Jr. amezaliwa tar. 27/9/ 1982 ni mshindi wa Tuzo za Grammy – akiwa kama rapa wa muziki wa hip hop bora kutoka nchini Marekani. Anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Lil Wayne. Alijiunga na studio ya Cash Money records akiwa bado yungali bwana mdogo na akabahatika kufanya rekodi kadhaa katika studio hiyo. Wayne alikuwa mmoja kati ya waliokuwa wanachama wa kikundi cha muziki wa rap cha Hot boys.

wyne amewahi kukaa jela mara kwa mara kwa kosa la miadarati na pia anapata sana matatizo ya degedege kutokana na matumizi makubwa ya madawa ya kulevya.

ALBAMU ALIZOTOA


1996-99
Alijiunga na kundi linaloitwa Hot Boys pamoja na juvennele,B.G na Turk walitoa albamu inayoitwa GET IT HOW YOU LIVE ambayo ilifanikiwa kuwa na nyimbo ambazo zilifika mpaka namba moja katika chart za billbord.

Albamu zungine ni kama;

1999–2002: Tha Block Is HotLights Out, and 500 Degreez

2003–06: Tha CarterTha Carter II, and Like Father, Like Son

2008–10: Tha Carter IIIWe Are Young Money, and Rebirth

2010–13: I Am Not a Human Being, Tha Carter IV, and I Am Not a Human Being II

2014–present: FWA and Tha Carter V
 
filamu alizoigiza;
2000 baller blockn.
2007 who’s your caddy?
2009 the carter
2009 hirricane season
 
 
 
Mtokambali 728x90

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *