Uncategorized

Aina nne za ujuzi wa mawasiliano unaotakiwa kujua na kujifunza

on

1. Sikiliza

Sikiliza kwanza, ongea baadaye. Heshima  huonekana pale ambapo tabia ya usikivu ipo kwako, sikiliza kisha utaelewa kitu, kama wewe ni mtu ambaye uoga huwa unakujia pale mfanyakazi mwenzako au bosi akiongea fanya kitu kimoja zima simu yako kisha sikiliza kwanza anachokisema mpaka mwisho baada hapo utaweza kumjibu bila woga wowote.

2. Lugha ya vitendo

Wewe kama kiongozi au unayeongozwa hakikisha unapowakilisha hoja yako unakuwa makini na vitu vifuatavyo Mgongano wa macho kati yako wewe na unayeongea naye, namna unavyoketi na pia muonekano wa uso wako hakikisha vyote hivi unavionyesha kwa ukarimu, heshima na furaha.

3. Kukabiliana na mabadiliko


Chunguza kwa makini mabadiliko halisi baada ya hapo kuwa mvulivu kwa sababu mabadiliko hayazoeleki kirahisi sana huchukua muda kuzoeleka.

4. Sema asante


Pale ambapo unakutana na marafiki zako, kiongozi wako au mwanafunzi wenzako sema asante pia pokea asante kwao hii huonyesha jinsi wewe unawasiliana kikarimu pia husababisha wenzako kuwa na ari ya kufanya kazi na kuona wanaweza kushinda chochote  kigumu.

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *