Cellebs

Mfahamu kwa undani msanii Shetta

on

Nurdin Ali Bilal amezaliwa mwaka 1990 katika jiji la Dar es salam hospitali ya Amana na kusoma katika shele ya msingi Boma na shule ya sekondari Benjamini Mkapa, Akiwa na umri wa miaka 20 aliweza kupata mtoto wake wa kwanza anayejulikana kwa jina Kyla pia mwaka 2017 aliweza kupata mtoto wake wa pili. Shetta ana mke na watoto wawili.

Kipaji chake cha muziki kilianza kuonekana mwaka 2009 baada ya kujiunga katika kundi la kucheza la Misifa Camp lilikuwa chini ya Msanii Prince Dully Sykes kisha kuwa kama back vocalist wa Dully katika show zake, baada  ya muda Shetta alijiunga na label ya muziki inayoitwa Dar stamina aliyokuwa chini ya SHABAHA pia mtu aliyemfanya mpaka apende muziki ni msanii Shabaha.

 

Alifanikiwa kutoa ngoma yake ya kwanza na msanii mkongwe wa hiphop Mwana FA iliyoitwa “Mi naplay” kisha baadaye mwaka 2010 baba Kyla alifanikiwa kutoa nyimbo ya pili ambayo ilikuwa ni hitsong yake ya kwanza iliyoitwa “nimechokwa” akimshirikisha Belle 9 nyimbo hii ilifanikiwa kumpa fursa ya kutumbuiza katika matamasha mbalimbali.

mwaka 2012 aliweza kutoa ngoma mbili ambazo ni “Mdananda” akiwa amewashirikisha dully sykes pamoja na Tundaman kisha “nidanganye” akiwa amemshirikisha msanii Diamond Platnumz, Aliendelea na kasi yake ya kutoa hitsongs na mwaka 2013 alifanikiwa kutoa ngoma na linah inayoitwa bonge la bwana kisha Sina imani aliyomshirikisha Rich Mavoko,

Mwaka 2014 alirudia kufanya ngoma tena na Diamond Platnumz iliyoitwa “Kerewa” nyimbo hii iliweza kumfanya shetta kuvuka mipaka ya Bongo kisha kuwa katika top chart za music katika bara la Africa ikiwemo kwenye vituo vikubwa vya TV kama  MTV na huko Nigeria na Africa kusini, Nyimbo hii ilimpa mafanikio mwakubwa hadi aliweza kusainiwa na record label kubwa africa inayoitwa Spice Africa kisha ikamtafutia dili la kufanya ngoma na msanii kutoka Nigeria Kcee kisha kutoa ngoma yao inayoitwa Shikorobo ambayo ilimfanya aweze kupenya zaidi Africa kimuziki,

nyimbo zake nyingine ni pamoja na Namjua, Wale wale na vumba aliyomshirikisha G nako.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *